Wanachepuka na hawakamatwi, why?

Wanachepuka na hawakamatwi, why?

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2009
Posts
8,597
Reaction score
1,690
Wao hawatumii simu kuwasiliana.
Msingi mkubwa wa wanaume wa aina hii wanatunza siri kuhusu wao wenyewe na familia zao, kazi zao hata majina yao wakati mwingine

HAWATUMII SABABU YA KUWA KAZINI
Mara nyingi mtu anaye cheat hutumia style moja ya kuwa kazi zinamfanya kuwa busy kumbe anatumia muda na hawala yake, hivyo basi wadanganyifu wa kiwango cha juu hawatumii sababu ya kuwa kazini kwani wanajua akianza kushtukiwa jambo la kwanza ni kuangalia muda anaotumia kazini.

HUHAKIKISHA MKE ANA FURAHA MARA ZOTE
Kwa kuwa atafanya kila njia kuhakikisha mwanamke anakuwa na furaha, hii ina maana kwamba mwanamke mwenyewe atajisahau na kujiona kuna amani kumbe ndani yake kuna udanganyifu mkubwa. Anaweza kukupa zawadi kila mara hasa akisafiri, anafanya kila kitu kuonesha anakujali kumbe anakuzunguka na inakuwa ngumu sana mwanamke kujua kwa sababu kila kitu anachohitaji anapata.

HAWATUMII SIMU
Wanaume wa aina hii si kawaida yao kuwapa mawahala namba za simu za mkononi, nyumbani au kazini. Wanajua kupitia simu za mkononi text message tu inaweza kuharibu mambo, acha kupigiwa simu kabisa. Pia wanajua wanawake ni rahisi sana likitokea jambo lolote ambalo hajaridhika au kukorofishana mara nyingi hupiga simu kwa wake wa hawa wanaume ili kuvuruga zaidi. Ndiyo maana hawatumii simu.

WANALIPA CASH BILA RISITI
Kawaida hawatumii credit card kulipia huduma zao kwani kuna bank huonesha matumizi ya pesa yako kwenye bank statement (hasa nchi zilizoendelea). Wanaogopa kwani kwenye account kunaweza kuonesha hotel na sehemu alienda na jinsi alivyotumia pesa.
Pia hawataki risiti kwani anaweza kujisahau akiwa nyumbani risiti ikakutwa kwenye mfuko wa suruali au wallet.

WANABANA MATUMIZI
Kawaida cheater mzuri hakopi pesa kwa ajili ya kustarehe na huyo mwanamke na pia anahakikisha matumizi yana balance na kuwa kama kawaida, hawana mambo ya ku-impress mwanamke kwa kutumia fedha nyingi hadi kukopa kwani wanajua matatizo ya kifedha yakitokea lazima atiliwe mashaka na kushikwa so mambo ya pesa wapo makini sana.

HAWADANGANYI OVYO
Hawana tabia ya kudanganya sana na mara kwa mara, kwani wanajua ipo siku data zitagoma bali wao huelezea uwongo unaofanana sana na ukweli ambao anayeambiwa anadhani ni ukweli kumbe ndani kuna uwongo.
Pia hawezi kueleza kitu hadi aulizwe pia anakuwa na majibu mafupi yasiyo na maelezo mengi ili kuficha data zaidi.

HAWATUMII MARAFIKI
Kawaida hawatumii marafiki au marafiki kuwasaidia kuficha siri zao. Wanajua marafiki kwa kuchemka au kwa makusudi wanaweza kufikisha habari kwa familia. Hujitunzia siri wao wenyewe na yeye tu ndo anajua kila kitu. Hata mwanamke ataambiwa asimwambie mtu na akimwambia mtu urafiki unakufa kwani anajua jinsi watu wengi wanavyojua issue basi uwezekano wa habari kuzunguka ni mkubwa.

WANAENDA MBALI
Kawaida cheaters wa aina hii si kawaida yao kutembea na majirani, marafiki, wasichana wa kazi au wafanyakazi wenzao au mtu yeyote ambaye yupo connected na mke wake, wao huenda mbali kabisa ambako hakuna mtu anawajua. Wanatumia ile principle kwamba ukiona mwizi anaimba jirani ndo kukamatwa kumekaribia, hivyo hawathubutu kuwa na wanawake wa karibu ambao jamii anaishi wanamfahamu.

KUMBUKA
Kuwa mwaminifu katika ndoa yako ndiyo jambo la misingi na muhimu si maisha yako tu bali hata familia, ukoo wako na jamii nzima.
Kumbuka kila mwizi ana siku yake ya arobaini hivyo basi hata kama hujagundulika ni vizuri kuacha hiyo tabia mapema ili uanze kujenga familia bora na yenye mafanikio pasipo wewe mwenyewe kuishi ndani ya guilt.

AMEN...........

Maelezo yooote hayo, lakini kumbe unazungumzia penzi la kahaba.....................!
Ni pale tu mwanaume atakapokuwa ana -cheat na kahaba ndio anakuwa kwenye usalama maridhawa wa kutokamatwa.
Makahaba huwa hawaulizi namba za simu, hawataki kujua kazi yako na wala hawana wivu............
 
Kimbweka kumbe sio jukwaa lileee tuu...aaah haya umeshawashika vipofu mikono:A S 465:. wataanza kuufanyia kazi ushauri wako.
 
Last edited by a moderator:
Ukishaamua ku'cheat' tu jua hauko salama..
Na hata kama utajidanganya kwamba haujulikani..amini iko siku moja utakutwa na punje ndogo ya wali kidevuni..na hapo ndipo mwizi wa wali atakapokamatwa!!..
 
hata ungekuwa smart vipi ipo siku mambo yatakuwa hadharani tu... ; and it could turn out to be so dramatic kama vile kukutwa gesti umepoteza fahamu juu ya kifua cha mtu..
 
hii mada ilitakiwa iwe sticky na strict for men,wadada haituhusu sie huwa hatucheat....:spy::spy:
 
wewe kula mzigo wa dada poa tulizana ila usinogewe...hakikisha dada poa ni wa mkoa mwengine
 
Yaani muda wote huoungetumia ku analyse why tanzania ina misitu lukuki lskini hatuna madawati shuleni we uko bize kuanalyse mambo ya ngono
 
Maelezo yooote hayo, lakini kumbe unazungumzia penzi la kahaba.....................!
Ni pale tu mwanaume atakapokuwa ana -cheat na kahaba ndio anakuwa kwenye usalama maridhawa wa kutokamatwa.
Makahaba huwa hawaulizi namba za simu, hawataki kujua kazi yako na wala hawana wivu............

Iwe ni kahaba, malaya au yeyote ni kwamba umechepuka na hujakamatwa
 
Yaani muda wote huoungetumia ku analyse why tanzania ina misitu lukuki lskini hatuna madawati shuleni we uko bize kuanalyse mambo ya ngono

Miaka yote 50 ya uhuru hakuna aliye analyse?
Kwanza unaelekea uelewa wako ni finyu kuhusu mazingira! Huna haja ya kukata misitu wakati tunaweza tengeneza madawati kwa kutumia plastic ama chuma, hiyo nimekupa kidogo tu...! Ngono ni sehemu ya maisha
 
Mh, umeshaharibu mkuu! Ngoja nimsikie wife atacomment nini...
 
aaaagh nilijisahau mkuu kumbe nimemwaga mchele kwenye kuku wengi.....?
Aiiiseeee.....!!!

Kimbweka sio siri umeniharibia sana! Wife keshaanza vituko na sipati picha leo atakavyoni audit, mwee! Nikikumbuka habari za poda ndo nachooooka!
 
Kimbweka sio siri umeniharibia sana! Wife keshaanza vituko na sipati picha leo atakavyoni audit, mwee! Nikikumbuka habari za poda ndo nachooooka!

Sasa tutalipozaje, lishabumbuluka hivyoo tenaaaa.........
 
Maelezo yooote hayo, lakini kumbe unazungumzia penzi la kahaba.....................!
Ni pale tu mwanaume atakapokuwa ana -cheat na kahaba ndio anakuwa kwenye usalama maridhawa wa kutokamatwa.
Makahaba huwa hawaulizi namba za simu, hawataki kujua kazi yako na wala hawana wivu............

Haswa kaka.......mambo yote ni CoD
 
ila wanawake wengi wanafahamu kuwa wanaume wengi wanacheat..........wanapenda japo umuheshimu.na unapomheshimu while cheating its obviously utakuwa makini huko.kwa maana ya kumlinda na kujilinda pia..............ila wale mnaojiachia kwa misimu,sehemu za starehe waziwazi nk ni kawaida kwamba utaku aunajiachia full ng'adu aka peku coz you dont care of whatever the hell infront of you...soma tena utanielewa
 
Maelezo yooote hayo, lakini kumbe unazungumzia penzi la kahaba.....................!
Ni pale tu mwanaume atakapokuwa ana -cheat na kahaba ndio anakuwa kwenye usalama maridhawa wa kutokamatwa.
Makahaba huwa hawaulizi namba za simu, hawataki kujua kazi yako na wala hawana wivu............

Haahaaa..haya mambo hayana tija kabisa
 
Back
Top Bottom