BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Uchumbaji wa michanga maeneo ya Mwaninga, Chekeni, Kisarawe II, Mwasonga, Kigamboni umekuwa ukisababisha zile sehemu zilizochimbwa kuwa kama visima na hivyo vyombo vya usafiri kushindwa kupita, hali hiyo inatupa changamoto kubwa kupata huduma.
Eneo letu hili ni la makazi ya Watu lakini sasa hivi limegeuka kuwa eneo la kuchimba michanga.
Tutukienda kuwasilisha malalamiko yetu kwa Viongozi wa Serikali za mtaa hakuna msaada wa maana, miundombinu umeharibika imekuwa ni sehemu ya Wachimba Mchanga.
Inapotokea kuna wagonjwa wa dharura au Wajawazito wanapopata shida ni mtihani kupata msaada, hada Bodaboda wenyewe wanaogopa kuja kutuchua kutokana na njia kutokuwa rafiki.
Ukitembea kidogo mitaa ya huku kujikuta umezama kwenye dimbwi la maji ni jambo ambalo linatikea mara kwa mara.
Wakati wa mvua Wanafunzi wamekuwa wakilazimika kukaa nyumbani kwa zaidi ya miezi kwa kuwa njia zinajaa maji inakuwa ni hatari kupita.