Wanachofanya ACT Wazalendo ni uthibitisho kuwa huwezi kupata Tume Huru ya Uchaguzi Bila kuwa na Katiba Mpya!

Wanachofanya ACT Wazalendo ni uthibitisho kuwa huwezi kupata Tume Huru ya Uchaguzi Bila kuwa na Katiba Mpya!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Msimamo wa Zitto Kabwe na ACT Wazalendo ni kuanza na Mchakato wa Tume Huru ya Uchaguzi halafu Katiba Mpya ipatikane baadae

Cha ajabu jana Zitto Kabwe kakimbilia Tunduru nchini Tanganyika na kuwataka Wananchi waamue kama ACT iendelee na SUK au ijitoe

Sasa unajiuliza SUK na Tunduru wapi na wapi?

Zanzibar Wana Katiba yao kwanini msimalizane hukohuko

Je, kwa kumteua Mkurugenzi wa Uchaguzi aliyekuwepo 2020 Rais Mwinyi amevunja sheria gani?

Wewe Zitto Kabwe wenzako walikuambia pigania Katiba Mpya hiyo Tume Huru ya Uchaguzi utaikuta humohumo, uwe unaelewa wewe Mkigoma

Alhamisi Ubarikiwe Sana!
 
Kosa kubwa la Zitto ambalo Kwa Sasa ameiambukiza ACT nzima ni kutaka kuifanya ACT adui wa CDM Mshirika wa CCM wakidhani itawabeba.

Malengo ya ACT ni tofauti mno na ya CCM. CCM wako tayari kufanya halali na haramu kubaki madarakani, ACT wanatafuta uwanja Sawa kihalali Kwa kusubiri huruma ya adui yao.

Kudhani kwamba Mambo yatajileta bila msimamo mkali ni Sawa na kusubiri embe chini ya Mbuyu. ACT Wana nafasi kubwa ya kupata wananchotaka wakisimama Kwa miguu yao, lakini wakitegemea huruma ya CCM mpaka 2040 hawataipata. Njia nzuri na Bora ni wanaoogopwa Zanzibar kuungana na wanaoogopwa Bara.

Wakijifanya wanafiki, wao hawana shida, tahamaki Uchaguzi huooo, na tume hii hii ya Mahela na Polisi wanaogombea vyeo CCM.
 
Back
Top Bottom