Kosa kubwa la Zitto ambalo Kwa Sasa ameiambukiza ACT nzima ni kutaka kuifanya ACT adui wa CDM Mshirika wa CCM wakidhani itawabeba.
Malengo ya ACT ni tofauti mno na ya CCM. CCM wako tayari kufanya halali na haramu kubaki madarakani, ACT wanatafuta uwanja Sawa kihalali Kwa kusubiri huruma ya adui yao.
Kudhani kwamba Mambo yatajileta bila msimamo mkali ni Sawa na kusubiri embe chini ya Mbuyu. ACT Wana nafasi kubwa ya kupata wananchotaka wakisimama Kwa miguu yao, lakini wakitegemea huruma ya CCM mpaka 2040 hawataipata. Njia nzuri na Bora ni wanaoogopwa Zanzibar kuungana na wanaoogopwa Bara.
Wakijifanya wanafiki, wao hawana shida, tahamaki Uchaguzi huooo, na tume hii hii ya Mahela na Polisi wanaogombea vyeo CCM.