Ni Shaloom Aleichim ni Kihebrew lugha halisi ya biblia. wao wanaishia shaloomAcha bifu zisizo na maana,
Asalaam alaykum ni salaam inulikanayo hata kweny bibilia, (tazama Luka 24:36) yaani yesu mwenyewe alitumia hiyo salaam,
ila wakristo wamekuwa wapingaji hawataki kuitumia badala yake mnaiona ni udini, Loh
Sent using Jamii Forums mobile app
Ila DSTV wananikosha mimi, yaani ndo maana sina mpango na king'amuzi cha aina nyingine kwa sasa.
Utakua mmoja wao wewe. Fanyeni kazi kwa akili acheni ujinga.Chuki binafsi maoni yako yako vizuri ila jitaidi kujificha na chuki dhidi yao
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mtangazaji wao mmoja wa mpira yeye ni asalamualeku tuu masaa yote sisi watizamaji hatuitaji itikadi zake azipeleke msikitini unaporusha kipindi kwenye jamii yenye michanganyiko ya imani jitahidi sana yale maneno uliyozoea kuyatumia kwenye imani yako usiyaongee utakwaza watu hata kufuatilia vipindi vyako. Hata kama neno hilo linamaana mzuri kiasi gani kwako lakini sii vyema sana
Azam hamna kitu.Azam tv nilitegemea wao wangekuwa watu smart kuliko kampuni zingine zote but kwa sasa naona wao ndio wamekuwa worse kabisa
Nimelipa kifurushi tangu juzi kabla hakijaisha coz nilijua kinaisha jana, lkn mpaka leo hii pesa imekatwa na kisimbuzi hakionesha, hakuna taarifa yoyote, huduma kwa wateja namba zote hazipatikani mabosi wao simu hawapokei
Sasa jaman huu si utapeli na wizi?
sijawah kuvutiwa na king'amuzi cha azam tangu kianzishweHama hao jamaa ni mbuzi tu. Ukiachilia mambo ya kulipia kisimbuzi wana ujinga mwingi ambao nime observe.
1. Jana katika kuonyesha mechi (sio jana tu) kuna muda ilifika tukawa tunaona wachezaji tu wakikimbia huku na huko ila mpira hauonekani. Nikajiuliza hao technicians wao hawalioni hilo. Director wa kipindi amesinzia au?
2. Zile mechi za ulaya ambazo huwa wanarusha kwa audio channel za Kiswahili wale jamaa wanao commentate hawajui mpira kabisa na nahisi hizo nafasi wanapeana kindugu. Yani vijana wapo mitaani tunajua mpira mpaka kero alafu wanapewa ajira watu ambao pamoja na kufahamu kuwa siku fulani watakuwa na matangazo ya mechi fulani lakini ni dhahiri kuwa hawafanyi hata maandalizi.
Kuna mechi niliangalia ya Liverpool vs Arsenal Carabao Cup iliisha 5-5 walikua hata majina ya wachezaji hawayajui, yani Neco Williams anampasia mpira Harvey Elliot lakini utasikia Elliot akitajwa kuwa ndio Williams na hata Elliot akimpasia Christie-Davis bado Christie-Davis wao watamtaja kuwa ni Williams.
Ile mechi kwakuwa audio channel iligome kubadilika kwenye english ilibidi ni mute [emoji347] tu niangalie bila sauti nikawasha sabufa nikafungulia singeli.
Kiujumla Azam walikuja kwa mbwembwe lakini kwasasa hawajui tu watu wanawakacha hamna wanaloweza. Kama ku adjust tu brightness hawawezi kuna nini kipya hapo?
Yule Baraka Mpenja nae anajiona sasa kawa commentator wa kiwango cha kina Peter Drury maana kila saa utasikia 'superb, what a hit, fantastic'. Mwambieni huku uswazi hatuelewi na yeye sio Peter Drury ni Mpenja.