Wanachokifanya Vipers SC Kwa Ceaser Manzoki, Ndicho Simba SC Walikifanya Kwa B. Morrison

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
View attachment 2294024
Hili sakata bado zito sana.

Ni mawili.

Subiri mwezi wa 10 ili umchukue mchezaji akiwa huru. Au peleka signing fee ya $100,000 ili chezaji apewe release letter na mukamilishe usajili wake.

Ujinga wanao ufanya Simba SC hapa ni huu:-

Wamefanya mazungumzo na wakala wa mchezaji ili waendw vipers sc wakajifanye kama wananunua mkataba ulio baki ili tu mchezaji awe huru. Gharama ya kununua mkataba wake ni takribani $48,000/= ila gharama ya kumnunua mchezaji ni takribani $100,000/=

Simba wameona ni gharama sana kumnunua mchezaji ukizingatia hali ya kiuchumi ya klabu na sintofahamu iliyopo klabuni.

Rais na tajiri wa Vipers SC amesema Manzoki ataindoka kama Vipers SC itapata offer nzuri zaidi au mchezaji akimaliza tu mkataba wake.

Mnakumbuka lile sakata la Bernard Morrison. Yes Yes ndilo linalojirudia hivi sasa.

WATABE MNASHINDWAJE KUNUNUA MCHEZAJI HATA WA KUTOKA HAPO UGANDA?

Na MLITEGEMEA VIPI KUMPATA ADEBAYOR?
 
Mchezaji mwenyewe anaonekana hataki kuendelea kucheza kwenye kitimu kidogo hicho ndiomaana tayari kasign pre-contract, sisi hatuna pressure kabisa tunajua mambo yatakuwa hivi.

Simba hawana namna inabidi wasubiri hadi mwezi wa 10 mkataba wake utakapoisha

"What comes around, Goes around"
 
Mchezaji mwenyewe anaonekana hataki kuendelea kucheza kwenye kitimu kidogo hicho ndiomaana tayari kasign pre-contract, sisi hatuna pressure kabisa tunajua mambo yatakuwa hivi.
View attachment 2294044
Naona wazee wa mseleleko mnajifariji! Wekeni 100,000/= mezani kama kweli mna jeuri.

Mpaka amalize mkataba mwezi Oktoba si mtakuwa tayari mshatolewa kwenye michuano ya Kimataifa na hao washambuliaji wenu butu.
 
Ukweli unajua kuhusu ambaye huwa anatoka mapema kwenye hayo mashindano.
 
Hujawahi kuona wachezaji wakinunua mikataba yao iliyobaki?

Ukiwa mshamba usilazimishe wengine waujue ushamba wako.

Mchezaji akiamua kwenda kushtaki FIFA habari itakuwa imeishia hapo.

Hao Vipers ni washamba kama mlivyo utopolo, na hili halina uhusiano wowote wa timu kuwa na pesa au kutokuwa nazo, ni matumizi ya akili tu.

Akili zile ambazo tulizitumia kuwakandamiza wakati ule mkimlilia Morisson.

Kumbuka, Simba SC kuna Mosses Phiri bado mpyaa hajatolewa kwenye box, na Augustine Okrah aliyeanza kuwanyoosha waarabu huko Misri hii leo.

#mtaumia
 
Naona wazee wa mseleleko mnajifariji! Wekeni 100,000/= mezani kama kweli mna jeuri.

Mpaka amalize mkataba mwezi Oktoba si mtakuwa tayari mshatolewa kwenye michuano ya Kimataifa na hao washambuliaji wenu butu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mbna umekua mpolee ghaflaa, vipi kimuhe muhe cha kumpokea DOMOLEPE kutoka Bifaso kimeishaaa?

Unavyoteseka sasa, woiiiiiiih

Byuti byuti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…