Hakuna ubishi kuwa S2kizzy aka Zombie ndiye producer mkali sana hivi sasa na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuachia hit songs tu na kujijengea heshima ndani na nje ya Bongo.
Hivi karibuni S2Kizzy alitangaza ku-record wimbo bure kwa wanafunzi wa chuo, na habari hii ilivutia umati mkubwa. Jana, wanafunzi wengi walijitokeza na kulala nje ya studio hizo za Pluto ili kupata fursa hiyo ya kipekee.
Your browser is not able to display this video.
Hali ilikuwa ya kusisimua, huku vijana wakisubiri kwa hamu kuweza kuingia na kurekodi sauti zao. Wanafunzi hao walionyesha ari na juhudi kubwa, wakiwa na ndoto ya kufanya muziki na kuonyesha vipaji vyao.
Your browser is not able to display this video.
Angalia ilivyokuwa: wahusika walipiga picha, wakisherehekea pamoja, na kila mmoja akijaribu kujiandaa kwa ajili ya kurekodi. Hii ni fursa ambayo wengi hawakuweza kuikosa, na inadhihirisha jinsi muziki unavyoweza kuwa daraja kwa vijana wa kisasa.
Hao wote walitakiwa wakapambane huko mashambani na viwandani,lakini kama mazingira na miundombinu ikiwepo .... sasa vijana kwa asilimia kubwa wakitaka kuwa wasanii hapo kuna shida