Wanachuo wajazana ofisi za Bodi ya Mikopo Dodoma

Nsoji go Nvaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2019
Posts
999
Reaction score
1,948
Katika hali ya kustaajabisha Leo June 1, 2020 mamia ya wanachuo kutoka vyuo mbalimbali mkoani Dodoma wameonekana wakisotea fedha zao za mkopo "Boom''

Hii imeleta sintofahamu maana Waziri wa Elimu ya Juu Mhe. Ndalichako alinukuliwa siku chache kabla ya vyuo kufunguliwa akisema kwamba mpaka sasa hakuna mwanafunzi anayedai fedha,wanafunzi wote fedha zao zimetumwa vyuoni

Sasa hii ya leo wanafunzi kujazana bodi huenda majina yalisahaulika au Waziri hakuwa na taarifa sahihi.
 
Hao wamefuata jela au masomo?? Hata siku ya kwanza tuu haijaisha wanapiga kelele, mmmh....
 
Kwani kujazana ni tabu sana waache wahakiki pesa, unataka waende Chuo bila uhakika wa payment
 
Picha Tafadhali!
 
Tatizo huwa ni wale ma'afisa mikopo wa vyuo husika.. huwa wana wacheleweshea wanafunzi mikopo kwa faida yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…