P h a r a o h
JF-Expert Member
- Mar 25, 2024
- 785
- 1,413
Nyuso za wanadamu zinazidi kuwa fupi zaidi, hii inasababisha kupoteza meno.
Kutokana na mabadiliko katika lishe, nyuso zetu zinapungua ukubwa, na tunakua na taya ndogo hii inamaanisha kuna kua na nafasi ndogo kwa menonkuota
Matokeo yake, watoto wengi sasa wanazaliwa bila baadhinya magego.
Kulingana na Dkt. Teghan Lucas wa Chuo Kikuu cha Flinders huko Adelaide, hii inaonyesha kuwa wanadamu bado wanabadilika —kwa kasi kubwa.
Dkt. Lucas na timu ya wanasayansi waligundua kuwa watu wanapitia aina fulani ya "micro-evolution," ambapo mabadiliko ya kiasili yanaweza kuonekana katika muda mfupi. Mabadiliko mengine yanajumuisha taya dhaifu, jambo linalohusishwa na utegemezi wetu mkubwa kwa moto na vyakula vilivyosindikwa kuliko hapo awali.
Wanasayansi pia waligundua kuwa baadhi ya watu wanazaliwa na mifupa ya ziada kwenye mikono na miguu, pamoja na mshipa wa damu wa ziada kwenye mkono. Pia walibaini kuwa baadhi ya watu huzaliwa na muunganiko usio wa kawaida wa mifupa miwili au zaidi kwenye miguu yao.
Utafiti huu umechapishwa kwenye Journal of Anatomy.
Hata hivyo, hii siyo tafiti pekee iliyofikia hitimisho kama hili.
soma zaidi:
Nature