Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Ndiyo group pekee ambalo wameweka kukaa nami miezi miwili. Wamejitahidi sana ila nadhani wamefikia hatua wameshindwa
Mimi mwenzenu haya magroup ya whatsapp huwa simalizi week moja. Wanani remove. Sijui wana matatizo gani? Admins wote wanafanana akili.
Mjadala ulianza last week kuhusu msiba wa ndugu yetu mmoja ambaye amefariki na wanataka akazikwe Bukoba. Wakati anaumwa hali yake ipo vibaya ila angalau... Nilishauri apelekwe kabisa Bukoba. Wakanijia juu kuwa why apelekwe huko.
Now kafariki imekuja issue ya kuchangishana kila mtu 500,000 kugharamia kukodi bus kubwa luxury na maiti kusafirishwa kwa ndege pamoja na watoto wake 4 na mama yao.
Nliwauliza kuna tija gani ya kulazimisha akazikwe kule? Je aliacha pesa ya gharama hizo? Je akizikwa hapa siku za mwisho hatofufuka? Kwa nini tuingie gharama hizo halafu baada ya hapo familia yake ibaki hoi? Maana watoto wake bado wanasoma.
Basi tuchangishane hizo pesa zikasaidie watoto wa marhamu. Imekuwa nongwa nimeshukiwa na kila mtu. Mimi sijaona wakijibu hoja wanadai tu ni mila n.k nikawauliza basi kwa nini isiwe sasa hata kwenye kuzaa mtu awe anaenda kuzalia huko huko kabisa.
Kifupi mimi haya magroup ya whatsapp nina gundu nayo. Juzi juzi nimegombana na jamaa yangu kani add kwenye group lake. Ila yeye tu admin ndo anaruhusiwa kupost. Sasa eti mimi niwe nasoma tu anachopost. Na yeye amekuwa motivational speaker. Anatuchosha tu na videos zake kila siku anaongea amekunja ndita eti kuonesha anaongea mambo sensitive. Nikajitoa. Kumbe na wengine nao baada yangu wakajitoa kutahamaki wamebak watatu katika watu 80 plus.
Amenijia juu kuwa kwa nini nilianzisha kujitoa na watu wametoka nami. Mambo mengine ni ujinga sana. Mimi ndo maana sidumu kwenye magroup sbabu siwezi kuvumilia upuuzi humo. Wanaona ni muasi. Wanani remove.
Sasa uje uniunge group lako kibwege bwege tu bila idhini yangu nakutolea mbavuni. Na hayo magroup yenu admins hamtaki kupingwa kaeni nayo huko huko.
Sasa hadi ndugu wananiona sifai kwenye magroup. Wakati huku JF watu wanaponywa kwa mchango wangu na madini aghali nayotema.