Wanafunzi 227 kutimuliwa UCLAS

Kubwajinga

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2008
Posts
2,193
Reaction score
299
Tuition pale Ardhi nafikiri ni kama TShs. 1,000,000. Matumizi ya JK NY kwa siku 10 kama atakuwa na entorage ya watu kama 10 hivi, itakuwa ni kama U$100,000. Hii inatosha 40% tuition fees ya wanafunzi kama 300 hivi.

Mheshimiwa raisi sijui atatueleza ni kwa nini hawa wanafunzi wanafukuzwa ikiwa yeye ameweza kuchomoa pesa za walipa kodi nyingi kiasi hicho? Hivi mzazi anaweza kutumia school fees ya watoto kwa ajili ya michango ya harusi?



Wanafunzi 227 kutimuliwa UCLAS

2008-09-23 11:20:36
Na Richard Makore


Zaidi ya wanafunzi 227 wa Chuo Kikuu cha Ardhi (UCLAS) jijini Dar es Salaam wameamriwa kufunga virago na kukatisha masomo yao endapo watashindwa kulipa ada.

Wanafunzi hao wanaosoma kati ya mwaka wa pili na tatu wametakiwa kuondoka baada ya kunyimwa matokeo yao ya mitihani hivyo kuwafanya wasiendelee na masomo kwa mwaka mwingine kwa madai ya kushindwa kulipa asilimia 40 ya ada.

Ofisa Uhusiano wa Chuo hicho, Alfred Mwanisongole alikiri wanafunzi hao kushindwa kulipa ada ya asilimia 40 wanayodaiwa.

Alisema awali wanafunzi hao walikata rufaa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kuomba kusamehewa kulipa kiasi hicho cha ada lakini waligonga mwamba.

Kutokana na hali hiyo, wao kama chuo alisema, hawana uwezo wa kuwasamehe wanafunzi hao na badala yake wanatakiwa kulipa ada ili kuendelea na masomo.

Aliliambia Nipashe kuwa maamuzi ya bodi hiyo ya kuwataka kulipa kiasi hicho yanatokana na fomu walizojaza wanafunzi hao wakati wanajiunga chuoni hapo.

Aliongeza kuwa Chuo hakiwezi kutengua maamuzi ya bodi hivyo lazima wanafunzi hao walipe ili waweze kuruhusiwa kuendelea na masomo.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi, Mwalembe Frank alithibitisha wanafunzi hao kutimuliwa chuoni hapo.

Frank alisema hawakubaliani na uamuzi wa bodi hiyo, hivyo wanatarajia kukata rufaa kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe.

Alisema awali idadi ya wanafunzi waliokuwa wamenyimwa matokeo ilikuwa kubwa lakini baada ya kuzungumza na uongozi wa chuo hicho, 228 walipewa matokeo yao licha ya kushindwa kumalizia kulipa ada na kwa wale waliofeli wameruhusiwa kurudia mitihani yao.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Profesa Maghembe alikaririwa akisema hakutakuwa na mabadiliko wala msamaha kwa watakoshindwa kulipa asilimia 40 ya ada.

Alisema lazima kila mwanafunzi alipe ada kulingana na fomu aliyojaza wakati anajiunga na chuo.

Jana serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, ilisitisha mgomo iliokuwa imetangaza kufanya baada ya wenzao 228 kuruhusiwa kuingia madarasani na kufanya mitihani ya marudio.

Uongozi wa wanafunzi ulipanga kufanya mgomo huo jana kama wenzao wangezuiwa kufanya mitihani ya marudio.
Kwa muda mrefu, kumekuwepo na msuguano kati ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini na bodi hiyo au uongozi wa vyuo vyenyewe.

Miongoni wa misuguano hiyo ni ile ya baadhi ya wanafunzi kushindwa kulipa ada kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za wazazi wao kutokuwa na uwezo.

Hivi karibuni zaidi ya wanafunzi 500 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliripotiwa kutakiwa kukatisha masomo kutokana na kushindwa kulipa asilimia 40 ya ada.

  • SOURCE: Nipashe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…