wanafunzi bora

Ms mashaba

Member
Joined
Dec 28, 2011
Posts
43
Reaction score
4
jameni nashindwa kuelewa kuhusiana na mafanikio wanayoyapata wanafunzi wetu. serikali yetu naona kama haiko makini katika kuwatambua mchango wa vijana hawa. miaka fulani iliyopita wanafunzi hawa walipewa zawadi nzuri kama vitabu, na wengine walipewa scholarship pamoja na kula dinner na raisi. but since mwaka 2007 sijawahi kusikia wanafunzi hawa wakidhaminiwa kama miaka iliyopita. lakini leo ndo nasikia wamepelekwa bungeni( form 6-2012).
je hapo kati kati serikali ilikuwa wapi?. inauma sana pale serikali inapofanya ubaguzi fulani.

mimi nilishashuhudia mmoja wa wanafunzi ilipata hamasa ya kuwa miongoni mwa wanafunzi bora miaka iliyopita. akajitahidi kweli akawa miongoni. but serikali yetu ilimvunja moyo kabisa kwani hakudhaminiwa kabisa.

ushauri wa bure kwa serikali wajitahidi kuwasaidia vijana hawa kwa hali na mali ili kufanikisha malengo waliojiwekea. Pia wapelekwe kwenye vyuo vya kimataifa na bora kwa sababu wakipata elimu bora watasaidia maendeleo ya nchi yetu.
 
Wewe sio mfuatiliaji ndio maana hujui
 
Kwa kumbukumbu zangu 2010 na 2011 walidhaminiwa pia sijui huko nyuma ila nadhani labda hawakutangazwa sana.
 
Wewe ni mwanafunzi bora? Km ni wa kike njoo nikupe zawadi unazotaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…