hii kwa kweli inanikumbusha mbali sana, kuna wengine walikuwa wana-wanyanyapaa wenzao kisa wanajituma katika kujisomea na kuwapachika majina eti "bundi","bunda","wametumwa na kijiji","wasongo" N.k
lakini ikifika wakati wa homework/assignment wanajipendekeza na wao wapate kubebwa. Pia kundi hili lilikuwa likishin kwa matumaini ya kuiba mitiani (almaarufu kama 'Feki') katika mitihani yao ya mwisho.
nachokiona mimi japokuwa sehemu kubwa ya tatizo ni serikali yenyewe kwa kuwanyanyasa Walimu kiasi cha kukinai kazi yao, huo ndio mrejesho wake, kubadilisha mitaara kila kukicha - kisiasa zaidi. Pia Kundi la hao hapo juu wasiopenda kujituma naona limeongezeka sana.