Wanafunzi Mlimani waandamana wakidai Katiba mpya

Wanafunzi Mlimani waandamana wakidai Katiba mpya

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Leo jioni kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku katika ITV wameonekana wanafunzi wa Mlimani wakiaandamana kudai katiba mpya, kupongeza hatua ya Bunge lao kuung'oa uongozi wa DARUSO na kusisitiza katiba mpya ni lazima itokane na raia wenyewe na wala siyo kukidhi mahitaji ya viongozi tu kupita Tume ya Raisi ambayo JK kaahidi kuiteua....................
 
binafsi nimeshatafuta katiba maana sipendi kujadili vitu bila kuelewa undani wake. nikimaliza kuisoma naingia kwenye mjadala huu kiufundi zaidi. nadhani kila mtanzania anaelewa kuwa katiba mpya inatakiwa kwa kuangalia tu utendaji wa serikali, bunge na mahakama.

mambo ni mengi lakini mifano hii ya karibuni yaani mauaji ya raia yaliyofanywa na polisi huko Arusha na Mbarali-Mbeya ni kielelezo tosha kwamba tunahitaji katiba mpya na mabadiliko makubwa ya sheria za nchi.

kwa hiyo ushauri wangu tuisome katiba vizuri ili tuijadili kwa upana unaotakiwa
 
Back
Top Bottom