Hullo, Wahandisi wetu Mlimani Chuo Kikuu. Bado migomo inaendelea au kuna utafiti mnaoufanya ? Wenzenu Nairobi wameiadapt dynamo ya baiskeli na wana kusudia kuwafikishia wanavijiji huduma ya kuchaji simu zao kwa kutumia baiskeli hizo hizo zinazotumika kwa usafiri.
KUBWA zaidi ni kuwa vijana hao wa Nairobi University sasa ni wajasiriamali na wenye kiwanda kidogo cha kutengeneza teknolojia yao hiyo iliyohitaji kutumia fikra na akili kidogo tu. Lakini kwa kuwa nyie hamtazami matatizo yanayowasumbua wazazi wenu bali kulalamika na kuandamana kila siku hamna muda wa kutumia akili zenu kujitajirisha wenyewe. Poleni sana! Na pole kubwa ziaidi kwa Watanzania maana wasomi wa namana hii hawatatupeleka kokote kule. Tutaendelea kuwa masikini hadi Yesu arudi tena!
Computer Centre shikamooni ? Toka muanzishwe mmeshagundua nini toka aliyoyafanya Kyaruzi ? Au mankwenda kwenda tu kiasi cha kushindwa hata kutoa vyeti vya wanafunzi wanaohitimu kwa wakati ? Kwa njia hiyo kweli mnaweza kugundua kitu?
Nimechoka na tabia yetu ya kuonesha kwamba ni juu tu mambo hayafanyi kazi kumbe na huku chini ni uozo mtupu. Amkeni Watanzania au mnasumbuliwa na ugonjwa gani usiotibika?
Uhandisi zaidi ya miaka ishirini mwashindwa kugundua pampu za maji, sindano, pasi, simu rahisi, redio rahisi, umeme wa sola na umeme wa upepo.Mmmmh ama kweli mna vichwa vigumu au rasilmali watu Tanzania ni tasa na gumba hasa!!!!