Sasa kuna changamoto imejitokeza hapa chuoni kwetu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ni kuhusu Wanafunzi ambao hawajapata mkopo mwaka jana (2023) na ambao waliokata rufaa.
Sasa kinachotokea ni kwamba Tawi la CCM Main Campus linawahamasisha na limetoa tangazo kwamba ili mtu upewe mkopo wa Bodi ya Mikopo (HESLB) lazima uwe na kadi ya CCM.
Na kupitia kwa kiongozi wao walichapisha kwenye magroup mbalimbali kwamba Mkopo na nyongeza (kwa wale waliopewa kidogo) watanufaika wale tu wenye kadi ya CCM na Wana-CCM kwa jumla.
pia soma ~
Wajumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa Wanaowakilisha Vyuo na Vyuo vikuu Taifa wafanya ziara Bodi ya Mikopo (HESLB)

Kutoka insta/X ya HESLB kule mata wa Jirani:
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI: UANACHAMA WA CHAMA CHA SIASA SI SIFA YA KUPATA MKOPO
Jumanne, Agosti 13, 2024
Tunapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii, likiwemo jukwaa la ‘JamiiForums’ kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) wanaoomba mkopo wanapaswa kuwa na kadi za chama cha siasa ili kupata mkopo.
Upangaji mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) unaongozwa na Sheria ya HESLB (SURA 178) na miongozo ambayo hutolewa kila mwaka kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili na kupatikana katika
www.heslb.go.tz
Sifa zinazotajwa na Sheria na miongozo ni mwombaji Awe Mtanzania; Awe ameomba mkopo; Awe amepata udahili katika taasisi inayotambuliwa na mamlaka za Serikali; Asiwe na chanzo kingine cha fedha cha kugharamia masomo; na kwa anayeendelea na masomo, awe amefaulu mitihani ya mwaka uliotangulia.
Aidha, miongozo inatoa kipaumbele kwa wahitaji kutoka katika makundi maalum kama yatima, wenye ulemavu na waliofadhiliwa katika masomo yao ya sekondari au stashahada ambao hupaswa kuthibitisha uhitaji wao kwa kujaza fomu maalum wakati wa uombaji.
Hivyo, miongozo ya mwaka wa masomo 2024/2025, kama ambavyo imekuwa katika miongozo ya miaka iliyopita, haitaji sifa ya uanachama kwa chama cha siasa kama kigezo cha kupata mkopo wa elimu ya juu.
Kwa msingi huo, tunawashauri wanafunzi wote wanaoomba mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali kupitia HESLB KUSOMA na KUZINGATIA miongozo ambayo ilizinduliwa na Mheshimiwa Prof. Adolf Mkenda (MB), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, siku ya Jumatatu, Mei 27, 2024 jijini Tanga na ambayo inapatikana katika tovuti ya HESLB (
www.heslb.go.tz).
Imetolewa na:
Dkt. Bill Kiwia,
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Jengo la PSSSF, Barabara ya Makole,
S.L.P. 984,
DODOMA