Jackal Malinza
Member
- Aug 28, 2013
- 33
- 4
WANAFUNZI VYUO VIKUU MMEWEKWA REHANI.
1.0. UTANGULIZI
Mfumo mzima wa elimu hapa Tanzania bado ni changamoto kubwa sana ya
kufikia malengo ya kitaaaluma na maendeleo ya kujitegemea kielimu.
Mfumo wa elimu ya Tanzania umejikita zaidi kuwafanya wanafunzi
wakimaliza chuo waajiriwe na si kuwapa mbinu za kuwafanya hata kama
watakosa ajira wanaweza kuwa wabunifu wa kubuni vitu vitakavyo wafanya
wajikwamue kimaisha. Pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali lakini
vyuoni kunamatatizo makubwa sana ambayo wanavyuo unapoongea nao
unapata huruma sana nahii ni kutokana na Serikali kuwa mbali na
matatizo ya wanavyuo, kwani shida kubwa zinazopatikana vyuoni si vyuo
bali ni wanavyuo wenyewe ,Nikiwa chuo kikuu nilikutana na hizi changamoto pia majadiliano na wanafunzi mbalimbali juu ya matatizo yanayowakabili
vyuoni na namna ya kuyatatua.
2.0. CHANGAMOTO VYUONI KWA WANAFUNZI.
Kuna changamoto nyingi sana ila tunalenga zile ambazo ndio zinazua
mitafaruku vyuoni;
2.1.MIKOPO
Serikali kupitia wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi hutoa mikopo
kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu Tanzania, moja ya fedha ambazo
hutolewa na bodi hii ni fedha za kujikimu, malazi, utafiti,ada kwa
asilimia n.k, kutokana na uwepo wa Bodi hii ya mikopo inaonekana kuna
ukritimba ndani ya Bodi na kuna siri kubwa nyuma ya pazia ambayo
tutaifichua siku si ndefu. Wanachuo wengi ni watoto wa wananchi wa
kawaida sana na hutegemea fedha kutoka bodi ya mikopo ili waweze
kuishi na pia wengine kupitia hiyohiyo fedha ya kujikimu huitumia
kumalizia kulipia ada vyuoni kulingana na asilimia au kiwango
anachopewa na bodi ya mikopo. Fedha hizi zimekuwa zikichelewa sana
kuwafikia wanavyuo husika kwa mda muafaka na hata sababu zinazotolewa
na viongozi wahusika hazina tija kwa maendeleo ya taaluma nchini maana
huwezi ukaweka programu ambayo haitekelezeki kikamilifu na kujikuta
wanavyuo wanaingia kwenye migomo kudai haki zao.
2.2. WANAOSABABISHA KUTESEKA KWA WANAVYUO NI;
2.2.1. BODI YA MIKOPO, bodi haina ukweli halisi katika kusaidia
matatizo ya wanachuo na wamekuwa wakiwapiga chenga wanavyuo, wanavyuo
wamekuwa wakiambiwa kama unaoona mkopo haujapata nenda bodi na
wakienda bodi wanarudishwa vyuoni bila kujua mstakabali wao zaidi ya
kuchezewa danadana. Wanapofanya migomo juu ya swala hili wanafukuzwa
vyuo.
2.2.2. UONGOZI WA VYUO(UTAWALA), kumekuwa na mkanganyiko mkubwa sana
baina ya utawala wa chuo na wanavyuo juu ya fedha kutoka bodi kwani
utawala wao hawajui kuhusu bodi wanachotaka ni fedha yao ulipe kama
unadaiwa. Utawala wa vyuo unalikimbia hili swala la mikopo ili kuepuka
migogoro na wanavyuo. Kimsingi vyuo bado vinanafasi ya kuwasaidia
wanafunzi wao ili kuwarahisishia kufanya vizuri katika masomo yao.
2.2.3. SERIKALI ZA WANAVYUO, hizi nazo zimeshindwa kazi viongozi
waliowekwa wanafisadi pesa za michango ya wanachuo kwani moja ya kazi
yao ni kushughulikia matatizo ya wanachuo wenzao hasa hili la bodi ya
mikopo na STUDENT UNION ndio nauli zao na posho zao katika
kushughulikia matatizo ya wanachuo lakini hakuna jipya bali serikali
za wanachuo zimegeuka ndio chanzo cha kusababisha wanavyuo kufukuzwa.
2.2.4. LOANS OFFICERS, hawa ni waajiriwa vyuoni wanashughulika na
maswala ya mikopo ya wanachuo lakini wamekuwa na majibu makali kwa
wanavyuo wanapodai haki zao na hakuna zaidi na wengine wanashutumiwa
kuomba rushwa ili kuwahisha mikopo.
2.2.5. MAWAZIRI WA MIKOPO VYUONI, hawana majibu sahihi kwa kuchelewa
kwa mikopo kila wanapotoa majibu yao ndio kwanza wanaweka siasa katika
maisha ya wanavyuo huku wao wakipata posho za safari.
2.3. MATATIZO YOTE YANAZALIWA NA BODI YA MIKOPO;
2.3.1. Wanafunzi kuandamana mara nyingi chanzo kikubwa ni fedha kuchelewa.
2.3.2. Wanafunzi kulawitiwa, kuibiwa na kuuza vifaa vyao.
2.3.3. Mgogoro wa wanavyuo na maeneo yanayowazunguka
2.3.4. Wanafunzi kuhisiwa kufanya biashara ya kujiuza.
2.3.5.Wanavyuo kuacha vyuo
2.3.6. Wanachuo kutofanya mitihani yao ya mwisho.
2.37. Wanavyuo kudaiwa walivyokopa kwa kusubiri bumu.
2.4.SULUHISHO.
Serikali haihitaji kuunda Tume wala kamati katika kukagua uozo uliopo
vyuoni, Bodi ya mikopo na wizara ya Elimu kabla hawajafanya selection
huwa wameshafanya majumuisho ya idadi ya wanafunzi watakaopewa mikopo
na bajeti yake kupitia wizara ya elimu hupitishwa bungeni, sasa ni
wapi na wapi tangu bajeti ipitishwe bungeni lakini wanavyuo wanalia na
bodi ya mikopo. Serikali inatakiwa kutambua bodi ya mikopo ni bomu
kubwa na siku likilipuka watakimbiana. Tunaiomba serikali ione uchungu
kwa Vijana wenzetu walioko masomoni lasivyo watasababisha migomo kuwa
mingi kama wataendelea kufumbia macho. Mwisho wa kuwahadaa wanachuo
umefika mwisho. Ni vyema viongozi wenye dhamana kushughulikia fedha za wanachuo kwani ziko kwenye bajeti yao na
wanapaswa kutekeleza mapema kwani ni haki yao.