Wanafunzi wa chuo Kenya waunda vifaa na kuuza China

Mungu atu saidie sana sija wahi kujua tatizo kati ya kenya na Tanzania especially pale wanapo jikuta wanachangia kitu cha maendeleo kilicho fanywa na moja kati ya nchi hizi. Sio challenge bali niku kashifiana tu hakuna ambae anaweza akajaribu kupongeza na kufanya mjadala kuwa wenye tuja ambao mwisho wa siku wote mna weza kufaidika. Tumesha rogwa na siasa kila kitu kupingana.
 
watz mna shida...Kitambo kidogo students pale jkuat wali design mkapayuka ati wameassemble...Hii nayo made in kenya fujo zishaanza...Mobius motors ilileta hii kashfa...Kibo bike vilevile..Tafuteni kitu ya kufanya mnabore sasa
 
Hongereni watani zetu,nchi zakiafrica zinatakiwa kukomaa kama hivyo.Tz tuna VETA na SIDO zinajitaidi kufanya innovation but still tunatakiwa kuwekeza zaidi kuvumbua nakununua technology mpya.Ngoja tuone nachuo chakimataifa cha technology cha Nelson Mandela kitatupa matokeo gani.Hongereni sana majirani inapostahili kupewa sifa inabidi mpewe
 
Wanacho fanya ni kuchonga spare parts kwa kutumia lathe machines kufatia michoro waliyo pewa na wachina basi.

Hawana furnances ya kuyeyusha chuma,shaba wala aluminium hawana pattern designing shop hawana forge/foundy shop hawana physical lab za kuchunguza microstructure za spare wala chemical lab za ku-analyse chochote,hawana shop ya kukomaza vyuma(heat treatment and quenching) hawana electroplating shop - kama huna shops tajwa hapo juu uwezi kuja hapa na kuzuga watu eti mnafyatua spare parts na kuwauzia Wachina!

Hayo mnaweza kudanganya watu ambao wana uelewa mdogo kwenye masuala haya, kinacho fanyika Wachina wanawaletea spare zilizokuwa forged kwenye mashop yao nyie mnacho fanya ni kuzichonga tu kwa kutumia lathe machines alafu mna re export kwenda China - Wachina wanacho tafuta ni cheap labor na kudumisha urafiki lakini sayansi yote ya kuhunda spare inabaki kwao Uchina, Wachina hawawezi kuwaleteeni/kuwajengeeni shops muhimu nilizo taja hapo juu.
 
Ni hatua lakini, Itafika hapo unaposema kuwa hawawezi kuwa wezesha na izo equipment s na Labs. Spendi kuamini kuwa it is impossible kama unavyo sema kila kitu kina wezekana hata china walianza hivyo.
 
at least wewe umeongea logic...
wengine wanatukana tu baada ya mtu kuwachallenge..

Hongereni majirani.

Ukitoa challenges za kipumbavu unajibiwa kipumbavu pia, nyie Watanzania mna hulka ya wivu na chuki za kichawi. Huwa mnaoneana wivu hata wenyewe kwa wenyewe na ndio maana ni vigumu sana kwenu nyie kupiga hatua yoyote pamoja na kwamba mna kila kitu.

Nakumbuka jamaa mmoja hapo Dar es Salaam, Mtanzania na mzawa kabisa, jamaa alikua mbunifu kiasi cha kunishangaza. Alikua fundi wa vifaa vya elektroniki na pia alikua na uwezo wa ku-design circuit board na kutuma Uchina ili vifaa vitengenezwe kwa design yake.

Sasa tatizo lilikua kwake yeye kupata biashara au hata wafadhili, kila tulipojaribu kumtafutia soko humo, alikua anapigwa chini na Waswahili wenzie kwa wivu. Hawataki kuamini kwamba Mwafrika, au hata Mtanzania wao atatoka kwa njia za ubunifu, tulijaribu kila njia hadi hata hapo COSTECH lakini alitamaushwa kishenzi. Anyway hatimaye alipata ufadhili nje ya nchi na sasa anapaa.

Huu uzi unahusu wanafunzi waliotengeneza vifaa na kuuza Uchina kwa milioni kumi za Kikenya. Ndio mara ya kwanza vifaa kutengenezwa Kenya na wanafunzi na kuuzwa Uchina. Sasa mijitu mliorogwa na wivu wa kufa mtu badala ya kutoa hongera mnaona mtafute sababu za kujipiga nyeto, eti hawakufanya design wao walitengeneza tu. Sasa hiyo ndio mnaita challenge huko kwenu.

Hawa wanafunzi wamedhihirisha jambo chanya, kwa mwendo huu wanaweza wakaibuka na kiwanda baadaye wakipata ufadhili wa kutosha na kuanza kutengeneza vifaa kwa ajili ya soko la Kenya na Afrika MAshariki. Cha msingi ni kwamba wamekidhi vigezo vya kutengeneza vifaa hadi vikauzwa nje ya nchi. Hivyo kesho itakua rahisi kwa wao kupewa design yoyote na kuitengeneza, sio lazima wao wafanye design.
 

Na hicho ndicho kinacho fanyika, lakini wenzetu hawa wakakuja na stori nyingi za kuchonga tu au labda ni kutokana na kutoelewa vizuri somo lenyewe hata sijui!!!!

Juzi juzi hapa walikuja na habari eti wanejipanga kununua trein 56!!! Nchini gani inahunda train? Nani kawambia train zinanunuliwa sokoni - Serikali/Taifa linanunua Locomotives na mabehewa hawanunui train - mnunuzi ndiye anafunga Loco na mabehewa mengi au machache apate train in otherword you form a TRAIN you don't buy a TRAIN.
 
Ni hatua lakini, Itafika hapo unaposema kuwa hawawezi kuwa wezesha na izo equipment s na Labs. Spendi kuamini kuwa it is impossible kama unavyo sema kila kitu kina wezekana hata china walianza hivyo.

Asante, hii ndio attitude inayofaa sio mijitu kuwa na wivu hadi hata dhidi ya wanafunzi. Afrika sasa hivi inaendelea kupata mwamko mpya, picha za dhiki walizokua wanaonyesha Wazungu zimeanza kudidimia na badala yake picha za matumaini ndio zimechukua usukani.
 
Ni hatua lakini, Itafika hapo unaposema kuwa hawawezi kuwa wezesha na izo equipment s na Labs. Spendi kuamini kuwa it is impossible kama unavyo sema kila kitu kina wezekana hata china walianza hivyo.

Mkuu yote niliyo taja hapo juu nimeyaona kwa wenzetu walio endelea sizungumzi nambo ya kubahatisha au kutaja ku underrate efforts za majirani zetu mimi natoa angalizo tu ili wajue what it takes kujiona unaweza kutengeneza spare parts za kukidhi viwango vya International Standards, wawambie Wachina wawajengee shops kama hizo hata kama ni kwa awamu - machining ya spare parts kwa kutumia lathe machine hatusadii sana kutuendeleza kisayansi/kitekinolojia, hayo ndio maoni yangu.

Sio kwamba Africa hakuna viwanda vya kufikia wenzetu Uchina na Ulaya - vipo mbona mfano mzuri ni Tanzania "TAZARA workshops Dar-Es-Salaam", karakana hii ni one of the biggest in Africa save South Africa and Egypt - unaweza kuhunda chochote kuanzia sindano mpaka a battleship - sio utani - wanasema na Mzinga ina uwezo huo lakini mimi binafsi na amini haiwezi kuifikia Karakana ya TAZARA.

Tatizo awamu za Serikali zilizo pita hazikiwekea maanani Karakana hii au kujali mambo ya sayansi na ufundi hasa sekta ya electro-mechanical, nguvu zao nyingi wanaelekeza kwenye masuala ya ICT mara e-Govt mara e-this e-that mradi William Gate kasema jambo fulani na sisi tunafuatia tu tunasahau mambo ya msingi - I hope JPJM ili atalifanyia kazi siyo anahacha a GEM kama karakana ya Tazara ifutike kwenye ramani ya bahati tuliyo kuwa tumepewa na Wachina!
 
wewe sio mgeni tena kwangu... nakufaham... hunipi shida.

waswahili husema.. "mbwa ukimjua jina......"
 
Kila kitu tuna cho na vyote hivi vilikua vinafanya kazi miaka mingi ilio pita. Vingi vime telekezwa na texhnilogia imebadikika kiasi kikubwa. Tatizo letu ni utashi wa viongozi kwajili ya kulisimamia hili swala na ndio kinacho tuangusha JPM ana nia jema kabisa ya kulitekeleza swala je vyuo vyetu ambavyo ni vya kiufundi viko tayari kuanda hao vijana watakao kuja kufanya kazi hizi. Ili kesho na kesho kutwa tujikute tun tengeneza na kuuza vifaa vyetu hapa hapa.
 
Juzi hapa Wanafunzi Wakenya walifanya design ya laptop halafu wakaituma Uchina ikawa assembled huko, mijitu mkaanza ule wivu ooohh! Ona wana assemble Uchina. Haya leo wanafunzi wametengeneza vifaa, mumeingia tena ooohh! hawakufanya design wenyewe. Aisei huyo Magufuli ana shida, mzee wa watu ana pressure kali sana kutawala watu wa aina hii, wasiojiamini na wenye wivu full. Sasa hivyo viwanda anaimba kila siku atavipokeza kwa nani kama mwendo ni kutamaushana kiasi hiki.

Japo kinachotia moyo Kenya ni kwamba wanafunzi wetu wanakijakaza, wanang'ang'ana, hawaskilizi upumbavu wa aina yoyote. Cha msingi tuendelee kuboresha wanafunzi wetu na ujuzi, ubunifu na ufundi, taratibu hao hao ndio wataibadilisha nchi kuwa ya viwanda kwa asilimia 100%
 
Ni hatua lakini, Itafika hapo unaposema kuwa hawawezi kuwa wezesha na izo equipment s na Labs. Spendi kuamini kuwa it is impossible kama unavyo sema kila kitu kina wezekana hata china walianza hivyo.

Nakubaliana nawe, kusema hawawezi kabisa ntakua nimekosea kidogo, lakini wakumbumbuke Wachina wa siku hizi tofauti na wa zamani - Serikali ya Kenya imeanza vizuri katika hili ila wajaribu kuwabana Wachina kwa kutumia lugha ya kidiplomasia ili wawajengee shops nilizo taja hapo juu ni za muhumi sana katika masuala ya spare parts na uhundaji wa vitu vingine vingi - hata kama watajenga kwa awamu - well and good. Sisemi haya kwa nia mbaya au kupotosha nina uzoefu wa kutosha.
 
chochote hata engine ya gari kinaweza tengenezwa hapa






alafu kuna hii campuni ya engeneering inaitwa seco, its the biggest in terms of ship building, overhauling, repaires in Eastern Africa .... watch the video in their website SOUTHERN ENGINEERING COMPANY LIMITED – MARINE & OFFSHORE ENGINEERING

Kenya airways wana kiwanda ambacho wanaeza tengeneza spare parts yoyote wanayohitaji for their commercial aircrafts. ..some evidence HOW KENYA AIR FORCE SET HISTORY BY REPAIRING JET FIGHTER OUTSIDE FACTORY


pia ukiskia tafuta habari za SGR uone wachina vile wanafanya 'skill transfer program' , wanapanga kujenga chuo kikuu cha reli ambacho wakenya na wanafunzi kutoka africa watasomea everything about rail building, hata mambo ya kutengenrza steel na ku test theire quality....

sasa jana walianza kutufundisha mambo ya utengenezaji wa chuma, leo hii wanatest wanafunzi wetu kuona kama wako sawa, kesho tutakua level nyengine, tunachohitaji sasa ni uwekezaji tu.. we ndelea kukaa hapo kama hater.... eti cheap labour..... cheap upuzi.....ofcourse sisi ni cheap labour by their standards, just like china is cheap labour by western standards..... sisi GDP/capita yetu ni ndogo, kwahivyo minimal wage yetu ni ndogo sana compared to them, but as far as we are concerned, its normal wage by our standards...... wacha wa outsource hizo kazi zote huku Kenya. .. we dont mind, as long as itatufanya tuondoke kwa agri-based economy tuende kwa industry based na employment level iongezeke hasa kwa watu wa chini...... there is no shortcut kwa hii game, dont expect tz itaanza kujiundia vitu na kuvitengeneza hadi kua serious manufacture bila kupitia hio curve......... sisi hapa kenya tumeonyesha lotencial kubwa sana, google brck ambayo ni made in USA designed in Kenya laptop ile ya jkuat ,..... just sit there and watch us rise from the bushes... hapa ndo silicon savanna!

Made In Kenya, Assembled In America: This Internet-Anywhere Company Innovates From Silicon Savannah
 
Unakera na hii matamshi , but sikulaumu. Kabla nikujibu ,nauliza ; hivi wewe una ufaham na industrial environment na maabara kwa ujumla zilizoko kenya?
 
I also didn't know there was this kind of thing btn Kenya and Tz. Because, back in highschool my bestfriend was a Tzian. I joined Jamii Forum thinking it would be the same.
 

Wewe ndiye unaongea kisomi, be blessed mkuu - ufafanuzi wako umejaa hekima sana - mkitumia mbinu tajwa hapo juu mtafika mbali sana, what counts ni kuwa na malengo na kufanya kazi kwa bidii na weledi, hilo tu ndilo linaweza kuwafanya wafadhili wa kutoa misaada ya vitendea kazi na mafunzo wawe na hamasa na moyo wa kuwasaidia.
 
Its true chief, Pia utawala bora wenye viongozi wenye utashi wamaendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla sio kujiangalia wao kwanza na familia zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…