Wanafunzi wa kidato cha nne na sita wataendelea kufeli

mwananchi wa pemba

Senior Member
Joined
Apr 2, 2013
Posts
129
Reaction score
80
Kama wote tunavyojua kwamba matokeo kwa miaka ya karibuni yamekua mabaya sana na kila mtu anataka kujua chanzo lakini nina WAHAKIKISHIA MATOKEO YATA ZIDI KUA MABAAYA ZAIDI kwasababu.

1] Serikali inajaribu kutafta njia ya kujisafisha machoni mwa watu lakin sio kulisafisha tatizo lililopo (kwa kuunda tume TUME wakati kila mtu anajua tatizo).

2]watu wanao enda kusomea ualimu ni watu walio shindwa katika elimu ( sasa watu walio feli wanaenda mfundisha mtu jinsi ya kufaulu).

3]walimu hawana mioyo ya kufundisha kwasababu ya mishahara midogo na maisha yanazidi kua magumu.

4]Siasa katika elimu;hapa ni serikali kujenga shule nyingi za kata wakati hawana ifadhi ya walimu so shule za kata ni makutanio ya watoto kupoteza mda ili miaka iende.

5]kupandisha alama za kufauru,,grades,,ndio tatizo kubwa.kama watoto iyo F YA 21 walishindwa vuka je ya 30 wataweza?

6]Utandawazi unao haribu watoto na kufanya nidhamu ishuke mashuleni..mtoto mdogo anachora madudu au ana andika matusi alaf hachukuliwi hatuwa.
 
mwenye akili haishii kulaumu bali na kutoa soulution.
 
Huwezi kutoa mapendekezo kwa sababu kama alivyosema mtoa hoja si kwamba tatizo halijulikani lakini wameamua kulifumbia macho. Hivyo, katika mazingira hayo hali ya elimu itaendelea kuwa mbaya na huenda NECTA wakafika mahali nao wakasema liwalo naliwe wakaamua kuonesha kuwa wanafunzi wengi wamefaulu kuliko uhalisia ili wasiendelee kupigiwa makelele. Hali ya shule zetu ni mbaya sana na walimu wanazidi kuvunjwa moyo kila kukicha.

Kwa siku zijazo manpower ya nchi itakuwa duni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…