DOKEZO Wanafunzi wa kidato cha tano kukataliwa kisa hawajamaliza michango ni usumbufu kwa wanaotoka mbali

DOKEZO Wanafunzi wa kidato cha tano kukataliwa kisa hawajamaliza michango ni usumbufu kwa wanaotoka mbali

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mawele

Senior Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
119
Reaction score
320
Habari, nawasalimi kwa jina la muungano......

Nina kero yangu haswa kwa shule za advance wanaopokea kidato cha tano walimu wakuu wanachukua maamuzi ya kumkataa mtoto kumpokea ikiwa tu hajamaliza michango na vifaa vingine kama vile vya usafi ukiangalia umbali uliotoka na mtoto ni mbali sana.

Pia soma:
  1. DOKEZO - √ - Shule ya Msingi Tumaini ya Tabata Kimanga Wanafunzi wasiochangia Tsh. 800 wanatolewa Darasani
  2. DOKEZO - √ - Malalamiko yaendelea kuhusu malipo ya 'Mchango wa Uendeshaji wa Shule Tsh 65,000' licha ya Serikali kufuta ada
  3. Wazazi wa wanafunzi Shule ya Sekondari BUJUNANGOMA, tumechoka na Michango, Rushwa, Utumikishwaji wa watoto wetu shuleni
  4. DOKEZO - Wanafunzi wa darasa la 7 shule ya Msingi Chanika wazuiliwa kuingia darasani kutokana na kutochangia 500 ya masomo

Mfano mimi mwanangu kupangiwa Kibaigwa Girls iliyopo Dodoma mwalimu mkuu na makamo Mkuu wa shule wamenigomea kumpokea mtoto kisa nimelipia nusu ya pesa za michango na sijakamilisha vifaa vya usafi ukizingatia nimetokea mkoa wa Mtwara sijui cha kufanya, naomba waziri husika kufuatilia hili jambo wazazi tunashindwa kuwapeleka shule mapema watoto kutokana na hizi changamoti. Naomba kuwakilisha🤝

Majibu ya Serikali, soma Serikali yaweka ukomo michango kujiunga kidato cha tano. Yaelekeza wanafunzi kutokataliwa kisa michango

Majibu ya Waziri wa Elimu; Waziri wa Elimu, Prof. Mkenda apiga marufuku Shule kuzuia Wanafunzi ambao hawajalipa fedha za michango
 
Back
Top Bottom