SoC04 Wanafunzi wa Kike na Elimu Tanzania

SoC04 Wanafunzi wa Kike na Elimu Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Antofrave

New Member
Joined
Apr 27, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Wanafunzi wakike nchini Tanzania wanapitia changamoto nyingi Sana katika masomo yao hasa shule za kijijini, changamoto hizi zinahusisha aidha familia(walezi), jamii inayomzunguka na walimu wake. Changamoto hizi hupelekea watoto wengi wa kike kupoteza masomo yao na kupelekea kufanya kazi wasizozitarajia baada ya kukosa msaada, mfano anaweza akapata ujauzito katika mazingira yakulawitiwa na mwisho wasiku akawa Hana msaada, anaamua kufanya kazi za baa, kazi za ndani ilihali mtoto apate mahitaji au kutelekeza pia watoto nakuendelea kujiuza kwa wanaume ili apate mahitaji ya maisha yake

Baadhi ya walezi mfano mwanafunzi anakaa na mjomba, babu yake au ndugu yake yeyote akishaona ameanza kupendeza mwanafunzi anatamani kumwingilia kimwili hivyo ili aweze kumlawiti kirahisi huwanyanyasa wasichana wakiwatishia wataacha kuwasomesha na kuwahudumia, hii inapelekea baadhi ya wasichana kuacha masomo yao kwa kulinda maisha yao zidi ya ubakaji au kuendelea kuficha ubakaji anaotendewa ili aweze kuendelea na masomo, hii Inaharibu saikologia ya mtoto wa kike na hata afikiapo wakati wakuwa na mahusiano anawachukia wanaume na pia kuathiri mfumo mzima wa utendaji kazi katika maisha yake,

Vilevile baadhi ya Walimu wanatumia njia ya kuwatishia kuwafelisha mitihani au kuwatengenezea makosa makubwa yakufukuzwa shule hivyo mwanafunzi anaamua kutembea na mwalimu wake ili kulinda Elimu yake iisipotee ili mradi akimridhisha mwalimu nakuharibu maisha yake, sababu kubwa ya mwalimu kufanya hivyo nikutokana na maisha duni aliyonayo anatamani angefika hata sehem za starehe apumzishe akili yake lakini uchumi haurusu hii inapelekea kufanya ulawiti kwa wanafunzi kwa kutumia vitisho

Na jamii inayomzunguka mwanafunzi hasa bodaboda na madereva wabajaji wanawapatia msaada wa lifti nakuwadanganya kwa urahisi Sana, na watu wengine wanavutiwa wakishaona mwanafunzi kanawili wanaanza kumdanganya na mwisho wa siku anaambulia maradhi na mimba za utotoni, hii inaathiri maendeleo ya nchi na ya wanawake, kwani mwanamke akielimika familia mzima itaelimika maana yeye ndo mwalimu wa kwanza kwa watoto wake

Kwa Tanzania tuitakayo naishauri serikali yetu iweze kuboresha mazingira ya wanafunzi wa kike kwa kuwajengea mabweni kuwasaidia wale wanaokaa na walezi wao wasilawitiwe, pia wasiweze kukutana na vishawishi vingi kutokana na jamii inayomzunguka, hii itwasaidia wanafunzi wengi kutumia muda wao mwingi kujisomea wakuwa mazingira salama pia wataipenda Elimu kwasababu hawatakutana na changamoto nyingi wanazokutana nazo mfano kutokupata chakula kwa wakati, na afikiapo nyumbani mzazi amemsubiria afanye kazi za ndani,hivyo akiwa mazingira ya shuleni atajisomea sawa na wanafunzi wanaopelekwa shule maalum.

Cha pili kwa Tanzania tuitakayo ninaishauri serikali yetu kuboresha mishahara ya Walimu ili angalau waweze kutimiza haja zao kwa watu wanaowahitaji bila kusumbua wanafunzi, maana kwa Sasa wengi wao wanaishi kwenye madeni makubwa hivyo mshahara wanaopokea unakuwa haukidhi mahitaji ya familia pamoja na starehe zao, badala yake wanaamua kumgandamiza mwanafunzi kwa kumtishia ili wawaze kupata wanachokihitaji kiurahisi, tukumbuke kuwa mwalimu ndo mtu wa kwanza wa kuliinua taifa letu tukimboreshea mazingira naye ataongeza ufanisi na ujuzi katika kujenga taifa letu, pia tukishindwa kumuinua akageukia upande wa pili atakuwa mtu wa kwanza kuiangamiza Tanzania tuitakayo maana Kila aliyejuu lazima apitie kwa mwalimu hivyo hatutaweza kupata wafanyakazi na viongozi Bora bila ya kuwa na walimu bora, nazidi kuishauri serikali iweze kuimarisha mazingira yake ili tuweze kupata matunda yaliyo Bora zaidi pia kuimarisha Elimu ya watoto wa kike maana Hawatasumbuliwa , mwalimu akiwa na Pesa yakukidhi mahitaji yake hawezi mnyemelea mwanafunzi kuharibu maisha yake

Cha mwisho naomba serikali iondoe utaratibu wakuwarudisha wanafunzi waliojifungua baada ya kupata ujauzito shuleni, hii inaathiri mfumo wa usomaji kwa wasichana kwa sababu hawatakuwa na hofu tena ya kumfukuza shule bali watahamasika kuingia kwenye mahusiano yasokuwa na tija wakiwaiga waliofanikiwa kurudi lakini tukumbuke siyo Kila mwanafunzi anayepata ujauzito anaweza akapata malezi Bora pamoja na mwanaye tukirejea zaidi kwa wanaotokea mazingira magumu na Elimu yao itaishia hapo, pia tukiwazuia tutapunguza idadi ya mimba za utotoni zinazopelekea vifo na watoto njiti, tuwasaidie wasichana au watoto wakike waweze kufikia malengo yao maana bila msaada wetu hawawezi kuyashinda majaribu kwasababu wao hufananishwa na embe au tunda lililoiva mtini litapigwa Kila aina ya mawe ili liweze kushuka , tunatakiwa tuwalinde ili tuvune matunda ya mawaziri, wabunge, Madaktari na wengine wengi na pia tunaweza kumpata Rais mwingine wakike ambaye atatufikisha kwenye Tanzania tunayoihitaji.

Bila kusahau vyombo vya usimamizi wa haki ya jinsia na watoto, waweze kusimamia haki za watoto wakike hasa kutoka kwenye familia zao , na serikali ishirikiane vyema kutoa adhabu kwa watu wanaolawiti watoto wakike na kuwapatia mimba za utotoni

Nahitimisha kwa kutoa ushauri kuhusu wanafunzi wote kwa ujumla wanaohitimu kidato Cha nne, baadhi yao wanapoteza mwelekeo pale ambapo serikali inawachagua moja kwa moja kwenda vyuo vya Kati na wanakuwa hawana chaguo la kwenda advance. Hii inakuwa ni ngumu kwa wanaotokea mazingira magumu hawana wakuwainua nakuweza kulipia gharama ya chuo, badala yake wanaamua kukaa mtaani na division II ama III.

Ushauri wangu nikuwapa chaguo wao Kama wanaweza kwenda advance au chuo ili nao waweze kuendelea namasomo. kwasababu akishamaliza advance anauwezo wakuomba mkopo kutoka bodi ya mkopo Tanzania, ushauri wa pili nikupunguza Ada ya vyuo vya Kati ili angalau wanafunzi wanaotokea mazingira magumu waweze kufikia malengo yao .

Nashukuru Sana kwa kutuletea story of changes naamini mawazo yangu yanaweza kuifikia Tanzania tuitakayo
 
Upvote 1
Cha pili kwa Tanzania tuitakayo ninaishauri serikali yetu kuboresha mishahara ya Walimu ili angalau waweze kutimiza haja zao kwa watu wanaowahitaji bila kusumbua wanafunzi, maana kwa Sasa wengi wao wanaishi kwenye madeni makubwa hivyo mshahara wanaopokea unakuwa haukidhi mahitaji ya familia pamoja na starehe zao
Hapo kwenye kushindana kumpatia mtu mshahara utakaotoshana na starehe ndio hakuna mtu wala serikali anaweza timiza.

Tusisitize yu mishahara inayokidhi mahitaji lakini kuhusu matakwa hapo ni juhudi za mtu binafsi. Na starehe mtu aliyoipigania ndiyo halali yake na mtu anaifurahia.

Kwa uzi huohuo nasisitiza ukiwa kama mzazi wapatie watoto mahitaji, lakini matakwa usiyasumbukie sana ni kuharibu kizazi cha kesho.

Kwa Tanzania tuitakayo naishauri serikali yetu iweze kuboresha mazingira ya wanafunzi wa kike kwa kuwajengea mabweni kuwasaidia wale wanaokaa na walezi wao wasilawitiwe, pia wasiweze kukutana na vishawishi vingi kutokana na jamii inayomzunguka, hii itwasaidia wanafunzi wengi kutumia muda wao mwingi kujisomea wakuwa mazingira salama pia wataipenda Elimu kwasababu hawatakutana na changamoto
Kujenga mabweni ni wazo zuri sana kwa kuwa inazo faida zake nyingi tu wanafunzi kukaa pamoja kwa lengo moja akili moja.

Lakini kwa maana ya kuwalinda kutokea nje tuu hatutafanikiwa, inabidi tuangalie na kuwaimarisha tokea ndani. Wawezeshwe kuwa na uwezo binafsi wa maamuzi, tabia shupavu na kuzikabili changamoto ndio tutakuwa na taifa la wawajibikaji.

Mengineyo tujitahidi kujifunza kwa wenzetu nje walipoendelea kuna kizazi kililelewa kwa kulindwa sana na mapendo ya hali ya juu na ma'helicopter parents' kilikuja kuwa changamoto hadi leo walishajifunza wanawalea watoto wao kwa upendo na akili.
 
Back
Top Bottom