Wanafunzi wa kike waua mwalimu wao... Adaiwa kutaka kumbaka mwenzao

Hii kitu hii, itauwa wengi.

huyu mwalimu naye yuo traditional mno..kwa nini asinunue bb awe anachat nao kwenye facebook ..mambo ya sijui njoo nyumbani madhara yake ndo hayo sasa...aaah pumzika mkufunzi wangu MAFINGO
 
KUna mengi hapo. Alijuaje kama hakulala bwenini. Ni obvious huyo mkufunzi anafanya kazi day and night including kukagua nani kalala bwenini nani hajalala bwenini. Kwa hiyo msimshangae binti kupeleka barua usiku. Inawezekana alimwambia usipoleta barua leo unafukuzwa chuo. Tukubali tukatae kuna wanaume wanatumua position zao vibaya kunyanyasa wanawake kijinsia. Inawezekana kwa kuwa aliona binti kalala nje basi akajua maharage ya mbeya maji mara moja kumbe mwenzie labda ana permanent boyfriend somehwere.

Najua kisheria binti yuko matatizoni ila simtetei huyo marehemu kirahisi kwani najua mazingira ya boarding na tabia za walimu wa boarding schools.
 
I dought hata kama ni kweli Mwalimu alitaka kumbaka au ni set up.

Hainingii akili kuwa Jean alipeleka maelezo ya maandishi kwa mwalimu nyumbani kwake tena usiku. My take ni kwamba kama kulikuwa na dalili za kumtaka kimapenzi huyo mwanafunzi basi Jean atakuwa alishaona hizo dalili na kwamba swala la kwenda nyumbani kwake usiku lingekuwa la hatari kwa maana ya exposure kwake? Nadhani kwa mwanafunzi kiwango chake asingefanya hivyo hilo linawezekana tu kama alipanga kumset huyo mwalimu...just speculating.
 
Inawezekana kabisa kuwa wanafunzi walishajipanga kumsaidia mwenzao. Nasema hivyo kwa kuwa mimi pia nilishakuwa mwanafunzi. Ila kujipanga huko kunaweza kukawa ni sababu ya mwalimu kumtaka huyo dada apeleke barua nyumbani kwake. Huyo mwanafunzi yawezekana amewambia wenzie mwalimu kanambia nipeleke barua home kwake usiku. Wenzake wakamwambia nenda akitaka kukubaka piga kelele tutakuja kumtia adabu! Kwa nini akupokea barua nje na kumwacha mwanafunzi aende zake? AU kama ni mwalimu wa nidhamu na anajua nidhamu kwa nini akumtimua na barua yake ili aipeleke kesho yake ofisini?

 
Amini tusiamini kwamba wote tulikuwa wanafunzi na ninakumbuka pia jinc walimu wa nidhamu wanavochukiwa, kutokana na adhabu aliyoitoa mkufunzi huyo, mwanafunzi yule alitakiwa kuyawasilisha maelezo yale muda wa kazi. Tujiulize
1. Kwa nini apelele maelezo usiku?
2. Kwa nini alipoingia tu apige kelele?
3. Kitu gn kilifanya urahisi wa wanafunzi hao kumpiga mkufunzi bila vithibitisho?



Tafakari! Chukua hatua, lazima kuna bifu la kibinafsi.
 

Duuuu hii kitu inaua watu sana, sio kwa ukimwi tu pia kipigo. Huyo kicheche ana kesi ya kujibu. Na mkuu wa shule ana kesi ya kujibu pia. Barua za nidhamu zinatumwa usiku? Na bylaw ya shule inasmeaje
 

kamanda angalia hapo nilipopaweka buluu kisha nisome hapo chini


1) Hii habari inasisitiza mara mbili kwamba "uamuzi" wa kwenda kwa mkufunzi usiku ni wa mwanafunzi na wala hakushurutishwa kwenda, ukisoma hapo buluu kwa umakini utagundua kwamba mkufunzi alimtaka mwanafunzi awasilishe maelezo ya maandishi ya kujitetea tu habari haikuonesha wakati wala mahala. Sasa mwanafunzi "anapoamua" kwenda kuwasilisha usiku tena nyumbani kwa mkufunzi inabidi tujiulize.

2) Habari inasema "mara alipoingia alianza kupiga kelele kwamba anabakwa", another weak point ,wataalam wanasema even crime need time and signs to happen.

3) Kama alivyoainisha mkuu MTM, hao waliovamia lazima walikuwa well organised kabla mavamizi, ni ngumu sana kuskia kelele tu tena nyumbani kwa mtu ukatoka straight na confidence ya kwenda kuuwa.

Lakini mengine yote ni mepesi , zito ni hapo habari inaposema kwamba ni uamuzi wa mwanafunzi kwenda kuwasilisha hayo maelezo usiku nyumbani kwa mkufunzi.
 
Dah! Hii kubwa.
Kwa maelezo ya mwanzo inaonesha huyu dada alisuka mpango na wenzake kama kumkomoa flani huyo ticha! ALIAMUA kupeleka barua ya maelezo NYUMBANI mida ya USIKU, alipoingia TU akaanza kupiga KELELE! Asingekufa huyo Dr wangeweza kuget away with it: kwa vile wamemuua, basi WATAJUTA MAISHA YAO YOTE kwa sababu wako likely zaidi kula nondo kwa kipindi kirefu tu, na hvyo future zao ZIMEVURUGIKA......!

Lakini hebu give me a break........., Kwani mwanafunzi wa chuo ni wa kuhangaikia kiasi cha kumzuia asilale nje?
 

Angalia vizuri hiyo sentensi kaka, kisha uirekebishe!
Kumbuka huyo alikuwa ticha, siyo kibaka kuwa atiliwe mashaka ya "KUBAKA"
Na kama kweli walijioganaizi hivyo basi hiyo ni organized murder, na WANA KESI YA KUJIBU MBELE YA PILATO.
 
kamanda, pamoja na signature yako kusema nisikuchukulie serious, on this one you are dead right!!!

This was choreographed na wanafunzi walipanga kumkomesha jamaa, the only problem ni kwamba walimpa zaidi ya walivyotegemea na hivyo kumuua...

Siku zote wanasema when a gang of youth wakipanga kitu, huwa ni hatari sana... cha kusikitisha ni kwamba the whole Bulongwa community walikua wapi?? vitu kama hivi havitokei overnight, huwa vinaanza na hoja, kisha majadiliano na kisha utekelezaji... where were the other teachers and students??? i dont believe kama ni wote ndio walioua, inawezekana kabisa hata outsiders walishiriki kukomoa bahati mbaya wakakua

very sad a young and educated man aliyejitolea kwenda bulongwa (sehemu ya mbali na mbaya kuliko Dar alipokua) kuuwawa kwa sababu ya nyege za watoto wa shule!!!
 



mimi naomba turudi kwenye ukweli pia,
je walimu wana tabia za kuomba ngono kwa kutumia cheo ?
jibu liko wazi ni ndio
hii habari kusema DENT aliamua kupeleka barua kwa ticha kweli inatia walakini kwa upande wa huyo mwanafunzi
lakini pia haya ni maneno ya nani? yawezekana ni muhandishi wa habari
jamii yetu ina CHALLENGE nyingi kufuata taratibu ni kama tunaogopa ukoma.
kwa mimi ninavyofikiria kama mwalimu angekuwa na mipaka katika ya kazi yake na masikini yake wanafunzi wasingepeka barua kwake.
SWALI GUMU, NI JE HIYO NI BARUA YA KWANZA KUPELEKWA HAPO NYUMBANI KWA MWALIMU USIKU?
 

wanaomba sana tu, ila soma upya mazingira ya tukio

Ukitaka undani nenda tu hata paleHospitali ya Ikonda Consolata (few meters apart) upate undani zaidi
 

Mkuu! the only source of information ambayo tunayo basi ni hii thread yako na ndio maana tunaibua masuali kutokana na thread inavyojieleza. Na kuhusu hapo red, Hilo tatizo kweli lipo lakini kisheria kila tatizo linahukumiwa kipekee kulingana na ushahidi unaowasilishwa, (hakuna ushahidi wa kwamba wengi wanafanya..... katika mahakama). All in all kwa habari ilivyowasilishwa basi nakuhakikishia huyo mwanafunzi kibao kitamgeukia tu, labda waje na masimulizi mapya.

Suala langu muhimu ni: Kwanini aliamua (rejea thread yako) kuwasilisha maelezo usiku tena nyumbani kwa mkufunzi?
 

hiyo kuamua hata mimi nakubali imekula kwake.
ila msingi ninaosimama nao mimi ni kwamba kumbe tunaweza kujiepusha na hila za wabaya wetu kama tukifuata taratibu.
kwa maelezo hapo juu ni wazi kwamba huyo mwanafunzi mvua imemnyeshea live.
ila mimi nadhani hii ichukuliwe kama changamoto kwa wafanyakazi wa sector zote
 
nimesikia kwamba huyo mwalimu alikua awe principal na wengi hawakupenda kwani alikua mnoko...

jiulizeni polisi walipata taarifa saa ngapi, mapanga wanafunzi waliyatoa wapi??

there were outside people as well
 
nimesikia kwamba huyo mwalimu alikua awe principal na wengi hawakupenda kwani alikua mnoko...

jiulizeni polisi walipata taarifa saa ngapi, mapanga wanafunzi waliyatoa wapi??

there were outside people as well

Nafikili kama watu wanaokufa kwa kupigwa au vifo vya ajabu ajabu polisi wangekuwa wanavichunguza kwa haki kama wanavyofanya wenzetu,
nadhani kuna watu wangekuwa JELA hii leo badala ya kuwa ofisini kama mabosi huku wakila bata.
bongo inatisha kuliko somalia,
maana adui yako umjui, unaishi kama mzima kumbe watu walishakuua wansubiri kukuzika tu
 
Huyo mwanafunzi kwa nini ameenda usiku kwa mwalimu? nahisi ni deal limepangwa tu
 
Huyo mwanafunzi kwa nini ameenda usiku kwa mwalimu? nahisi ni deal limepangwa tu

katika hii post utata huko hapo kwenye hiyo, mimi najiuliza je ilikuwa mara ya kwanza barua kupelekwa usiku kwa mwalimu
 
katika hii post utata huko hapo kwenye hiyo, mimi najiuliza je ilikuwa mara ya kwanza barua kupelekwa usiku kwa mwalimu
Hivi jiulize huyo msichana aliitwa kupeleka usiku huo hiyo barua au alitaka kumkomesha prof wa watu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…