SoC02 Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaoshindwa kufaulu mitihani ya taifa wapewe nafasi nyingine ya kurudia mitihani hiyo

SoC02 Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaoshindwa kufaulu mitihani ya taifa wapewe nafasi nyingine ya kurudia mitihani hiyo

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 2, 2022
Posts
60
Reaction score
75
Chapisho hili lina lengo la kutoa ushauri kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kuhusu Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaoshindwa kufaulu mitihani ya Taifa wapewe nafasi nyingine ya kurudia mitihani hiyo badala ya kurudia darasa au kidato kwa mwaka mzima.

Utangulizi, Mitihani ni njia ambayo Mwanafunzi au Mtu anapimwa kutokana na alichokisoma au alichofundishwa ili atambuliwe kwamba alielewa au hakuelewa. Au kwa maana nyingine mtihani ni kipimo cha maisha kutokana na ulichojifunza. Katika shule mwanafunzi hupimwa na walimu wake juu ya kile walichomfundisha ili kumjua kama alielewa au hakuelewa. Ili mwanafunzi afaulu mitihani yake inampasa asome kwa bidii.

Kwa Tanzania Wanafunzi hufanya mitihani mbambali ikiwemo mitihani ya nusu muhula, muhula wa kwanza pamoja na muhula wa pili na mitihani ya Taifa ambayo ipo chini ya uangalizi na usimamizi wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) mitihani hiyo kwa kawaida hufanywa na Wanafunzi wa darasa la nne, darasa la saba, Wanafunzi wa kidato cha pili, Wanafunzi wa kidato cha nne pamoja na Wanafunzi wa kidato cha sita. Mitihani hii hutungwa na baraza la mitihani na hufanyika nakusahihishwa na baadae matokeo hutolewa chini ya usimamizi na uangalizi wa baraza hilo la mitihani.

Baada ya matokeo kutangazwa na Baraza la Mitihani, Watahiniwa waliofaulu kwa daraja linalotakiwa huendelea na darasa lingine au kidato kingine, na watahiniwa walishindwa kufaulu mitihani kwa daraja linalotakiwa hawaruhusiwi kuendelea na darasa lingine au kidato kingine badala yake hurudia darasa au kidato alichokuwa anasoma mwanzo, hii ni kwa watahiniwa wa darasa la nne na kidato cha tatu lakini kwa watahiniwa wa darasa la saba, wa kidato cha nne pamoja na kidato cha sita walioshindwa kufaulu mitihani yao mara nyingi huchukuliwa kama wahitimu hivyo huendelea na maisha mengine ya mtaani labda mwanafunzi mwenyewe aamue kwenda kusajili kama mtahiniwa wa kujitegemea au arudi tena kujiunga na shule ili awekeze kurudia mitihani yake iwapo kama akifaulu aendelee na ngazi nyingine ya elimu.

Mfumo huu wa Watahiniwa wa shule za msingi na sekondari wanaoshindwa kufaulu mitihani yao kurudia mwaka mara nyingi huwavunja moyo Wanafunzi na wengi wao hukata tamaa ya kuendelea na masomo kwani huwa wanaona kurudia darasa alilokuwa anasoma awali ni kupoteza muda na umri . Kwa mfano kuna baadhi ya wanafunzi ya hujikuta wanazeekea shuleni kwa kurudia darasa. Hivyo basi kwa nini Baraza la Mitihani Tanzania lisibadili mfumo na kutumia mfumo unatumika vyuoni.

Kwa kawaida vyuo vikuu Tanzania mwaka mmoja wa masomo huwa na mihula miwili na kila muhula huwa na mitihani ya muhula (Semister Exams) na baada ya matokeo kutoka watainiwa waliofeli huwa hawarudii mwaka bali huwepewa nafasi ya pili ya kurudia mitiahani ambayo hufahamika kama (Supplementary Examinations). Na watainiwa walioshindwa kufanya vizuri katika mitihani ya muhula wanapopewa nafasi ya kufanya mitihani waliyofeli asilimia kubwa ya watainiwa hufaulu mitihani hiyo ya marudio. Iwapo kama mtahiniwa atashindwa kufaulu mitihani hiyo ndio hurudia mwaka wa masomo kwa somo aliloshindwa kufaulu.

Kwa nini mfumo unaotumika vyuo vikuu Tanzania usitumike kwa watahiniwa wa shule za msingi na sekondari? Au wanavyuo hufeli kwa bahati mbaya na Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hufeli kwa makusudi, kama jibu ni hapana,

Basi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wapewe nafasi ya kufanya mitihani ya marudio pindi wanaposhindwa kufanya vizuri katika mitihani ya awali kama ilivyo kwa wanachuo. Siku zote Kutenda Kosa sio kosa ila kurudia Kutenda kosa ndio kosa hivyo basi kwa nini Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walioshindwa kufaulu mitihani ya Taifa wasipewe nafasi ya pili ya kurudia mitihani hiyo. Badala ya kurudia darasa au kidato kwa mwaka mzima.

Kwa sababu watahiniwa wanaposhindwa kufanya vizuri katika mitihani yao haimanishi kuwa hawana akili au hawazingatii wanachofundishwa na walimu wao darasani. bali kuna sababu nyingi za kushindwa kufanya vizuri. Kwamfano baadhi ya watahiniwa wanaweza wakawa na matatizo ya kifamilia, matatizo ya kiafya, pamoja na sababu nyingine zizopo nje ya uwezo wake na kuwafanya washindwe kujianda vizuri kwa ajili ya mitihani.

Hivyo basi ninaimani kama watahiniwa walioshindwa kufaulu mitihani ya kwanza wakipewa nafasi ya kurudia kufanya mitihani kwa masomo waliyoshindwa kufanya viruzi wataweza kufanya vizuri badala ya kurudia kusoma mwaka mzima. Mwanafunzi atatakiwa kurudia m waka iwapo kama atashindwa kufaulu mitihani ya marudio kwa daraja la ufaulu linalotakiwa.

Mwisho, ninashauri Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) liachane na mfumo wanaoutumia kwa sasa ambao watahiniwa wanaoshindwa kufaulu mitihani yao hurudia darasa au kitado kwa mwaka mzima kwani mfumo huu. huwavunja moyo Wanafunzi na wengi wao hukata tamaa ya kuendelea na masomo kwani huwa wanaona kurudia darasa alilokuwa anasoma awali ni kupoteza muda na umri. Pia wazazi na walezi huingia hasara ya kurudia kulipa ada pamoja na michango mingine kama mwanafunzi atakuwa anasoma shule binafsi za kulipia.

Badala yake Baraza litumie mfumo unaotumika vyuo vikuu kwa kuandaa mitihani mingine ili kuwapa watahiniwa walioshindwa kufaulu fursa ya kurudia mitihani kwa masomo waliyoshindwa kufanya vizuri. Kwani mfumo huu unafaida mbalimbali ikiwemo watahiniwa husika walioshindwa kufanya vizuri kwenye mitihani ya awali watapata nafasi ya kurekebisha makosa yao ya awali, mzazi au mlezi wa mtahiniwa ataondokana na gharama za kurudia kulipa ada na michango mingine hususani kwa watahiniwa wa shule binafsi, na matumizi ya serikali pia yatapungua kwa sababu hakutokuwa na idadi kubwa ya Wanafunzi wanaorudia darasa au kidato.

Pia, mfumo huu hukoa muda kwa wanafunzi kwa sababu hawatorudia kidato au darasa kwa mwaka mzima bali hurudia tuu mitihani kwa masomo aliyoshindwa kufanya vizuri. Faida nyingine ni kuongezeka kwa idadi wa watu waliosoma katika Taifa.

Maana ya maneno yaliyotumika;

Mtahiniwa (wingi watahiniwa): mtu anayepimwa uwezo wa kujibu maswali ya mtihani.
 
Upvote 8
Nime kupigia kura !!!

Kuhusu suala la kurudia mitihani ni kwamba mwananfunzi lazima arudie darasa ndiyo aje apewe mitihani tena.

Mwanafunzi inapotokea kafeli inamaanisha ajaelewa alichokuwa anafundishwa kwahiyo suala la mwanafunzi kurudia mitihani pindi anapo feli bila kuingia tena darasani siyo sahihi.

Na mwanafunzi kurudia darasa inawezekana ni maamuzi yake mwenyewe endapo akirudia basi lazima baadae hata kuja kufanya mtihani mwengine.
 
Ni kweli kaka lakini kwanini mwanafunzi wa vyuo vikuu huwepewa nafasi ya kurudia mitihani waliyofeli bila kurudia mwaka mzima?
 
Ni kweli kaka lakini kwanini mwanafunzi wa vyuo vikuu huwepewa nafasi ya kurudia mitihani waliyofeli bila kurudia mwaka mzima?
Kwanza ningependa kujua elimu yako ?

kurudia mtihani bila kusoma ulicho kosea kwenye mtihani kwa uelewa wako unaona ni sahihi.

Kama mtu amefeli utaratibu wa kurudia mitihani upo kwenye level zote za elimu Tanzania yani kuanzia chekechea mpaka chuo wote wanayo nafasi ya kurudia mtihani sasa.

Unacho takiwa kujua ni kwamba mtu anapo fell mtihani anakuwa ajaelewa chochote mtu huyo utawezaje kumpa mtihani mwengine bila ya kumsaidia kwa kumlekeza yani kumfundisha upya kabisa alafu ndiyo uje kumpa mtihani mwengine.

Kwahiyo mtu aliye "feli" inamaanisha ajaelewa alichokuwa anafundishwa darasani lazima ajifunze kuanzia upya hapo ndiyo atakizi vigezo vya kufanya majaribio ya kile alicho jifunza.

Kwa lugha nyepesi mtihani maana yake ni majaribio ya kile MTU alicho jifunza, kwahiyo mtu ambaye ajajifunza hafai kupewa mtihani lazima asome na kujifunza kwanza sijui umenielewa.
 
Mm ni mhitimu na chuo tulipokuwa tunafeli tulikuwa tunapewa mitihani ya kurudia (supplimentary exams)kwa mitihani tuliyokuwa tumefeli bila ya kurudia mwaka mzima, baada ya kufeli mtihani wa marudio ndio ilikuwa inatubidi turudie mwaka mzima.
 
Kwanza ningependa kujua elimu yako ?

kurudia mtihani bila kusoma ulicho kosea kwenye mtihani kwa uelewa wako unaona ni sahihi.

Kama mtu amefeli utaratibu wa kurudia mitihani upo kwenye level zote za elimu Tanzania yani kuanzia chekechea mpaka chuo wote wanayo nafasi ya kurudia mtihani sasa.

Unacho takiwa kujua ni kwamba mtu anapo fell mtihani anakuwa ajaelewa chochote mtu huyo utawezaje kumpa mtihani mwengine bila ya kumsaidia kwa kumlekeza yani kumfundisha upya kabisa alafu ndiyo uje kumpa mtihani mwengine.

Kwahiyo mtu aliye "feli" inamaanisha ajaelewa alichokuwa anafundishwa darasani lazima ajifunze kuanzia upya hapo ndiyo atakizi vigezo vya kufanya majaribio ya kile alicho jifunza.

Kwa lugha nyepesi mtihani maana yake ni majaribio ya kile MTU alicho jifunza, kwahiyo mtu ambaye ajajifunza hafai kupewa mtihani lazima asome na kujifunza kwanza sijui umenielewa.
mbona kimya
 
Back
Top Bottom