Imekuwa ni tabia kwa baadhi ya madaktar wa ngazi ya juu zaidi hususani wakati wa kupitia wagonjwa asubuhi(ward round) kuwafukuza wanafunzi wa ngazi ya chini diploma nakuwaambia wasubiri walimu wao kitu ambacho sio sahihi kwani wagonjwa sio kwa ajili ya masters au degree au diploma pia kumekuwa na tabia ya baadhi ya manesi kutumia lugha za ukali kwa matabibu wanafunzi (clinical officers) mbele ya wagonjwa hivyo kupelekea wagonjwa kutowaamini wanafunzi hao wakati wakuchukua maelezo. Nanukuu kutoka kwa daktar mmoja "NAOMBA NIBAKI NA WATU WALIOVAA TAI TU YAAN WANAOSOMA (MEDICAL DOCTORS)MD" DIPLOMA WOTE NJE.
Naomba kuwasilisha hayo. Pia ikumbukwe tatizo hili halijaanza leo.
Hii ni tofauti kabisa na hospitali nyingine kwa namna inavyowachukulia wanafunzi wa diploma kama vile hispitali ya rufaa ya manyara, hospitali ya wilaya ya kongwa n.k kuhusu matatizo ya kiutawala na vyuo husika hakuna changamoto vyuo vimekuwa vikipambana sana wanafunzi kupata mafunzo hapo general hospital