Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema wanafunzi wa VETA, ambao leo Machi 15, 2025, wamefanya ukarabati kwenye wodi ya watoto ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, ikiwemo kupaka rangi, wamekuja kuonesha uwezo wao kutokana na yale wanayojifunza VETA.
"Sisi tunafurahi kwamba wenzetu wa VETA, katika Maadhimisho ya Miaka 30 tangu VETA ianzishwe, wamejipanga kuonesha shughuli ambazo wanaowafundisha wanaweza kufanya. Mojawapo ni kupaka rangi katika maeneo mbalimbali, ambapo sehemu kubwa ni hii (Muhimbili), lakini najua watafanya na Iringa, Tabora, kwenye mashule, zahanati na hospitali," amesema Prof. Mkenda.
"Wanafunzi hawa wanaposoma VETA wanafundishwa vitu vingi, mojawapo ni ujenzi pamoja na kupaka rangi, kwa hiyo wamekuja kuonesha uwezo wao," ameongeza.
Pia, Soma: Waziri Mkuu Majaliwa: Wenye degree kasomeni ufundi VETA mjiajiri
Prof. Mkenda ameyasema hayo wakati wa hafla ya ukarabati wa wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, uliofanywa na wanafunzi wa VETA kuelekea Maadhimisho ya Miaka 30 tangu kuanzishwa kwake.
Chanzo: TBC Digital