Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Gambaia waandamana kupinga hali duni za masomo

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Mamia ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Gambia (UTG) jana Oktoba 26, 2026, waliandamana wakipinga kuzorota kwa mazingira ya masomo, changamoto za upatikanaji wa chakula na huduma duni za intaneti.

Waandamanaji hao walikusanyika katika chuo hicho kilichopo Banjul, mji mkuu wa Gambia, wakilalamikia changamoto mbalimbali zinazoathiri shughuli zao za kitaaluma, zikiwemo usafiri usiokidhi mahitaji, upatikanaji mdogo wa maji ya kunywa na kufungwa kwa mgahawa wa chuo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Wanafunzi wa chuo hicho iliyotolewa Oktoba 25, 2026 Wanafunzi pia wanakabiliwa na huduma zisizoaminika za intaneti pamoja na kukwama kwa shughuli za masomo. Wakati wa maandamano hayo, wanafunzi walisikika wakipaza sauti wakisema, “Tumechoka.”

Maandamano hayo yamefanyika wiki chache baada ya maandamano mengine yaliyochochewa na kukatika mara kwa mara kwa umeme nchini humo.

Wizara ya Elimu ya Juu ya Gambia imesema imepokea malalamiko ya Wanafunzi na kusisitiza umuhimu wa mazungumzo ya kujenga, ikikiri kuwa madai hayo yanahitaji ufuatiliaji endelevu, uratibu mzuri na suluhisho la vitendo.

Oktoba 24, 2026, Serikali ilitangaza hatua kadhaa za kushughulikia malalamiko hayo, ikiwemo kurejesha huduma za chakula kuanzia Jumatatu, kuongeza sehemu za kupata maji ya kunywa, kuboresha usafiri na kuimarisha huduma za intaneti.

Chanzo : Eyewitness News, Jambo TV


​
 
Mamia ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Gambia (UTG) jana Oktoba 26, 2026, waliandamana


Africa sijui nani ambae amaetuloga, ila hii yote inatokana na mifumo hasi ya uongozi nikiwa na maana kuwa system ya uongozi ipo corrupted to exitent ambapo viongozi hawaoni shida za waongozwaji ila wanachokifanya ni kuangalia maisha yao binafsi, nchi nyingi za kiafrica hazina mipango mikakati ya mda mrefu na hili ndio shida.
 
Kwahiyo ufaransa pia wamerogwa?

Uchumi hauhitaji hasira
 
Wapinzani walishinda uchaguzi 2016 wakijua kuwa kuendesha nchi ni rahisi sasa hivi 2026 kinachotokea hawakiamini

Tafuta uzi umo humu walishinda uchaguzi kwa kutumia goroli kama sikosei ndio zilitumika kupigia kura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…