mwaka huu wizara ya elimu imetunga mtihani wa darasa la saba wa mtindo wa multiple choice kwa masomo yote ikiwemo hisabati/hesabu, na hivyo kurahisisha kuibia majibu, kukisia majibu na kuweza kushinda hata kwa bahati tu za kudra ya mtu. Kwenye mtihani wa multiple choices yenye majibu manne kwa kila swali likiwemo jibu moja sahihi kila mtoto ana 25 % chance ya kupata jibu sahihi hata kwa kukisia tu. Kama wizara inabisha basi ifanye jaribio uitoe nakala za mitihani hii kwa machinga, wapiga debe, etc pale ubungo stend na wawachague wale ambao hawakuweza kuvuka darasa la nne wawape huo mtihani, si ajabu ukapata pass rate ya 75 % au zaidi just by sheer lukcy. Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!!