Hapa JK wala si wa kulaumiwa. Tatizo ni moral compass ya Prof Mukandara tu. Yeye kama mzazi anapaswa kufikiria walichogomea hao watoto ni cha msingi, ila navyofahamu, kama siyo yeye basi wanawe au wajukuu zake watakuja kukutana na mkono wa hao walioathirika na ndiyo watakapo tambua kuwa kumfukuza mtu chuo si jambo la maana. Unajua hao vijana waliofukuzwa wanaweza kwenda kujitoa muhanga na kumuua? Inauma sana jamani, maana maisha ni magumu, shule ndiyo inapaswa itoe unafuu kwa hao vijana, then wanawafukuza, ni taifa gani hili? Yaani viongozi wa Tanzania ni wabinafisi sana, hawapendi wenzao wapate maendeleo, ni sawa na hao waliowafutia matokeo darasa la saba, wanataka waende wapi? kwa nini hao watoto darasa la saba wasifundishwe maadili (ethics) ya kuibia mitihani? kwa sababu naamini wao na walimu wao pia hawafahamu, tena usikute waalimu ndiyo wachochezi wa kuvujisha mitihani, then leo wanaadhibiwa tu hao watoto, je wahusika wakuu? Bongo ujinga mtupu!