Wanafunzi wanafeli kwa kung’ang’ania Kiingereza

Wanafunzi wanafeli kwa kung’ang’ania Kiingereza

mkada

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Posts
1,200
Reaction score
907
WAKATI wananchi wakisubiri kutangazwa na kuundwa kwa tume ya kuchunguza chanzo cha wanafunzi wa kidato cha nne kufeli, Kaimu Katibu wa Mufti Zanzibar, Sheikh Thabit Noman Jongo, amesema chanzo kikubwa ni serikali kuendelea kukubali mitaala ya elimu ifundishwe kwa Kiingereza badala ya Kiswahili. Sheikh Jongo ametoa kauli hiyo jana kwenye mahafali ya tatu ya Jukwaa la Vijana wenye imani tofauti za dini Zanzibar lililofanyika kwenye ukumbi wa Ecrotanal mjini hapa.

Alisema mfumo wa mitaala ya ufundishaji unaotumika Tanzania ni wa ajabu kwa kuwa wanafunzi wanafundishwa toka darasa la kwanza hadi la saba kwa Kiswahili na baadaye wanapojiunga na sekondari hufundishwa kwa Kiingereza, hali inayowafanya washindwe katika mitihani.

"Mataifa makubwa yaliyopiga hatua kimaendeleo kama China, Japan, Urusi na Oman, wanafunzi hufundishwa kwa lugha zao za asili na sasa iweje kwa Watanzania kushikilia Kiingereza ambacho si lugha ya taifa?" alihoji.

Alisema somo la Kiingeraza katika nchi hizo huwa si lazima na kusema katika nchi kama Uganda unaweza kumkuta mtu anaongeza Kiingeraza lakini hajui kuandika. "Wanafuzni wanaojaza michoro kwenye mitihani nafikiri hawafanyi kwa bahati mbaya, upeo wao hugota ukingoni wanapoikabili mitihani iliyotungwa kwa Kiingereza," alisema sheikh huyo ambaye anakaimu nafasi ya Sheikh Fadhil Soroga aliyemwagiwa tindikali Novemba 6 mwaka jana.

Akizungumzia matukio ya kuhujumiwa kwa viongozi wa kiroho Zanzibar, Sheikh Jongo alisema yanatisha na hayakubaliki katika imani za dini zote. Alisema vitendo hivyo vimejaa ukatili kwa sababu hakuna dini inayoagiza kuua bila ya sababu na kuvitaka vikosi vya vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina kuwasaka wahalifu hao.

"Hali tunayoiona Zanzibar ni ya kushtusha, hatujui chanjo cha kutokea kwa matukio hayo kama yana sura ya kisiasa au dini, hatutaki amani ipotee na watu kuhasimiana kwa ajili mitazamo ya kiimani," aliasa Sheikh Jongo. Alisema kitendo cha Serikali ya Tanzania kukubali kuleta wapelelezi ni sahihi, kwani anaamini itasaidia kutegua kitendawili hiki na wahusika kukamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya sheria. Sourece Tanzania Daima Feb 03,13.
h.sep3.gif
 
Huo sio ukweli. Mbona somo la kiswahili nalo wamefeli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1. Somo ambalo hufundishwa kiswahili tangu elimu ya kindagaten. Shule za msimgi masomo hufundishwa kwa kiswahili.mbona nako watoto wanafeli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Hujapata jibu sahihi, endelea kutafuta.
 
hio research imefanywa na sheikh mkuu.
 
aliesema hivyo ni kiazi;material karibia yote yanaandikwa kwa ngeli...iweje kiwekwe kando??????
 
Back
Top Bottom