Wanafunzi wanakaa kwenye vituo vya daladala kwa muda mrefu

Wanafunzi wanakaa kwenye vituo vya daladala kwa muda mrefu

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Serikali ikiendelea kupiga hatua dhidi ya uboreshaji wa elimu Tanzania mkoa wa mwanza unakabiliwa na changamoto wanafunzi kukaa mda mrefu kwenye vituo vya magari kwa kukosa kipaumbele mda wa jioni hasa kipindi cha mitihani ya taifa.

Adha hiyo hutokana na wanafunzi kutokupewa kipaumbele cha usafiri mda wa jioni kusababaisha wanafunzi kukaa mda mwingi kwenye vituo vya magari.
Changamoto kama hizo husababisha uchovu na kusababisha wanafunzi kukata tamaa kwani hawapewi kipaumbele ukizingatia wanao toka kwenye mtihani yao.

changamoto hizo zimeshudiwa hivi karibuni wanafunzi wa kidato cha pili wakiomba msaada kwenye kituo cha usafiri natta lakini kondakta hawakutia maanani.

Kuelekea mitihani ya kidato cha nne serikali inatakiwa kuchukua hatua ili kuhakikisha wanafunzi wanapewa kipaumbele hasa majira ya jioni pindi wanapo toka kufanya mitihani.
vilevile serikali inatakiwa kutoa elimu sahihi kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri nyakati za mitihan wanafunzi wanatakiwa kupewa kipaumbele ili kuondoa changamoto zinazotokea.

Hali imekuwa ni endelevu hata kabla ya mitihani kwani daradara zimekuwa zikiwaacha katika vituo jambo ambalo huweza kuwaathiri kitaaluma.

Vilevile kipindi cha asubuhi huchukua mda mrefu kufika shuleni hivyo inakuwa changamoto kwao serikali inatakiwa kutoa elimu sahihi kwa lengo la kusaidia wanafunzi wanapokuwa katika masomo yao.
 
Wengine wanapata kisingizio hicho hicho kuchelewa usafiri kumbe wanakwenda kugegedana na wenzao

Ova
 
Hapo Kuna wanafunzi waondoe maana huwa wanangoja gari yenye mziki plus kutega tega wafike home baadae
Ila usumbufu huwa upo na ndio maana serikali inajitahidi kuongeza shule za kata watoto wasiende umbali mrefu ila nao waache kuchagua magari hasa vya Pugu station sec
 
Back
Top Bottom