Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 7,093
- 10,469
Hivi tufanye nini hasa kwa Wanafunzi ambao huwa wanaboreka sana darasani? Mimi ni mfano hai wakati niko shule na ni ngazi zote kuanzia Shule ya msingi mpaka Sekondari nilikuwa naboreka sana darasani na saa nyingine nilikuwa nasinzia na kuamshwa na viboko, na sababu kubwa ni kwamba kile alichokuwa anakifundisha mwalimu nilikuwa nakijua tayari hivyo kwangu ilikuwa ni kama Mwalimu anafanya marudio tu na matokeo yake ni kusinzia!
Sasa hili tatizo naamini kuna baadhi Watoto au wanafunzi pia wanalo huko Mashuleni, sasa ni nini kifanyike kwa hawa Wanafunzi wanaoboreka Darasani, kwa maana unaona kama Mwalimu anakupotezea muda vile, na Mtihani ukija unauona ni rahisi sana, sasa tufanye nini?