ksksk
JF-Expert Member
- Aug 24, 2022
- 301
- 713
Kumekuwa na tatizo kubwa kati ya makondakita wa hizi dalaldala na wanafunzi wa shule za msingi na sekondali kwa walioko mbali na shule zao unakuta mtoto kawahi kuamka hata saa 11 asubuhi ili awahi usafiri asichelewe shuleni anafika kituoni hata saa 12 kasoro hivi akiamini amewahi usafiri lakini inakuwa tofauti na matarajio yake .
Magari mengi yakifika makondakita hawawataki wanafunzi waingie kwa magari yao mpaka unajiuliza hawa hawana watoto!! na kama wanao huko mashuleni wanakosomea watajisikiaje siku wakiona watoto wao wanafanyiwa haya na ni muda wa kuwahi shuleni ,muda mwingine unakuta konda hana tatizo sana lakini dereva wake ndio hataki au muda mwingine dereva hana tatizo lkn konda wake ni shida sana .
Naziomba mamlaka husika zipige jicho huku kwa umakini watoto wengine unakuta ni umri mdogo wako hata madarasa ya chini wakati huo muda tunaamini hao ndio viongozi wa baadae huko wa taifa hili ,watoto wakifika shuleni wamachelewa kule napo kuna taratibu zake inapelekea wengine kukosa baadhi ya vipindi kutegemea adhabu atakayokutana nayo siku hiyo nasisitiza sana hili limulikwe kwa umakini sana watoto ni wetu na tuwajali, tuwapende, tuwathamini lakini pia tusiwafanye wakue na visasi mioyoni mwao kesho na kesho kutwa Mungu anamsaidia mtoto anafanikiwa kuwa hata daktari ndio tunaona hatendi sawa na taaluma yake au kitengo chochote kile lkn anakuwa hatendi kama anavyopaswa kuwa kumbe moyoni kayabeba mateso mengi huko nyuma nawasilisha

Upvote
0