Wanafunzi watoro waadhibiwa kwa kufungwa kwenye mti, Walimu wakuu matatani

Wanafunzi watoro waadhibiwa kwa kufungwa kwenye mti, Walimu wakuu matatani

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Kikosi kazi cha mashirika mengi kimeamuru ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kitaanzisha uchunguzi kuhusu tukio la walimu wawili wakuu katika Shule ya Msingi ya Thiru huko Laikipia Magharibi nchini Kenya wanaodaiwa kuwafunga wanafunzi watatu kwenye mti kama adhabu. Televisheni ya Citizen nchini Kenya imeripoti.

Kikosi kazi kinachoongozwa na naibu kamishna wa eneo la Nyahururu Moses Muroki alitumia siku ya Jumatano kusikiliza maoni ya walimu na wanafunzi kuhusu tukio hilo lililotolea Ijumaa iliyopita.

Bw. Maina anashutumiwa kuwafunga kwa kamba kwenye mti wanafunzi watatu Ijumaa iliyopita ikiwa ni adhabu kwa kutega shule, kabla ya kuwapiga picha ambazo zilisambaa mitandaoni.

Inadaiwa kuwa baadaye alizituma picha hizo kwenye kundi la WhatsApp la walimu kabla ya mmoja wao kuzivujisha picha hizo kwenye mitandao ya kijamii. Televisheni ya Citizen ilieleza.

Tukio hilo sasa linafanyiwa uchunguzi na mamlaka zimesema hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya walimu hao iwapo watakutwa na hatia.

IMG_20210902_085129.jpg

Chanzo: BBC
 
Kuna kipindi walimu nao wanavurugwa hadi wanapandisha mashetani.
 
Kama malezi ya shule unapokuwa mdogo yanaanza hivi je ukiwa mkubwa inakuwaje,hapa sasa ndio napata picha kwanini majirani zetu wakenya mko hivyo mlivyo...
 
Yaani kusoma kunalazimishwa. Shule inatakiwa iwe ni mazingira rafiki kwa mtt mpaka ajisikie amani akiwepo pale shuleni. Sio Kama gerezani. Yaani
 
Back
Top Bottom