Elli, unachosema ni kweli kabisa, na kwa kweli nashangaa michango ya wengi kwenye hii mada. Sijui labda wengi humu wamekuwa mashuleni miaka ya 60, 70 na 80, sijui miaka hiyo hali mashuleni ilikuwaje. Lkn miaka ya 90 na kuendelea haijalishi umesoma day au boading, ukisema hukuona au hujui 'vituko' vya wanafunzi, ni ajabu. Wanafunzi 'kuwatega' walimu na wanafunzi wenzao, kutumia vibaya fursa za kwenda tuition, likizo, weekend nk. Tukifumba macho na kujifanya hatuoni kuwa wanafunzi wengi wanamiliki simu ambazo wazazi/walezi hawajui (na nyingi ni za bei mbaya.) Tukifumbia macho ukweli kuwa vyombo vyetu vya habari (magazeti wanayopata zaidi ni ya udaku) vipindi vingi vya radio na tv ni vya kuwapotosha. Tukijilazimisha kutokuona tatizo kuwa ratiba na majukumu ya wazazi wengi wa mijini ktk taifa hili haviwapi mda wa kutosha kuwa na watoto wao. Tunapoendelea na utamaduni wa mwanaume wa miaka 30 mwenye afya na nguvu kukaa kwenye siti ya daladala na mwanafunzi wa miaka 10 akiachwa kubanana na watu wazima akiwa amesimama bila kumhurumia... Wanafunzi wanaponyanyaswa na kuzuiwa kupanda kwenye daladala na tunaona sawa, Tusishangae kusikia makubwa zaiadi ya waliyofanya hao watoto.