Wanafunzi wawili wa shule ya upili Kenya washinda tuzo la U.N. kwenye maonyesho na mashindano ya kisayansi na 'project' iliyowagharimu KES 100

Wanafunzi wawili wa shule ya upili Kenya washinda tuzo la U.N. kwenye maonyesho na mashindano ya kisayansi na 'project' iliyowagharimu KES 100

pingli-nywee

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
11,923
Reaction score
13,350
rqpmqrmbarapohsti5b1b6d12e53a7.jpg
Esther na Salome wakiwa na mwalimu wao Peter Tabichi ambaye alishinda tuzo la mwalimu bora duniani 2019.~ Wanafunzi wawili wa shule ya upili ya Keriko Secondary School Nakuru, Kenya wameshinda tuzo la U.N. Sustainable Development Goal Award. Esther Amimo na Salome Njeri, na project yao ya 'Essameter', walifika kwenye fainali ya maonyesho na mashindano hayo ya kisayansi, ISEF yaliyokuwa kule U.S.A., na yanayodhaminiwa na U.N. Project yao ambayo iliwagharimu KES 100 tu ni kifaa kitachowasaidia vipofu na viziwi kupima 'distances', 'angles' na kwenye somo la hesabu pia. Mradi wao uling'aa kwasababu uliambatana na SDGs za U.N. Yaani Sustainable Development Goals ambazo zinanuia kubadilisha maisha ya walemavu duniani.
ktsuvabyn50etg6sh5cdf150997048.jpg
https://www.standardmedia.co.ke/article/201326003/kenyan-school-girls-sh100-invention-wins-un-award
 
safi kabisa
esther_amimo_and_salome_njeri_at_the_international_science_and_engineering_fairisef_0.jpg
Sana. Hawa wanafunzi ni wabunifu kupindukia na wameiwakilisha nchi yao ya Kenya vilivyo. International Science and Engineering Fair(ISEF) ni mashindano ya kimataifa ya kisayansi yanayowashirikisha wanafunzi 1,800 kutoka nchi 75 duniani! Wadhamini wa mashindano hayo ya kila mwaka ni U.N., kupitia shirika lao la U.N. Science and Cultural Organisation na ndio mashindano makubwa kabisa ya kisayansi kwa wanafunzi wa shule za upili duniani. Hiki kifaa chao 'Essameter' ambacho jina lake limeunganisha majina yao Esther na Salome ndio walishinda nacho kwenye 56th Kenya National Science & Engineering Fair 2019. Wakenya waliofuzu kwa mashindano hayo ya kimataifa yaliyokuwa kule U.S.A mwaka huu ni wanafunzi kumi kutoka shule tatu nchini.
 
Hongera zao, elimu ya Kenya inazidi kupaa.
Kweli kabisa, ni kiashiria kizuri kwamba kuna mengi mazuri yanayoendelea kwenye sekta ya elimu Kenya. Hawa ni wanafunzi kutoka shule ambayo sio maarufu sana kule vijijini. Ila wamefanikiwa kutumia vitu vya kawaida kwenye mazingara yao, kwa gharama ya shilingi mia tu, kubuni kifaa ambacho kitabadilisha maisha ya walemavu wengi. Hiki kifaa chao cha Essameter ni 'callibrated' na kina alarm, ambayo inalia 'target' ikifikiwa. Kando na kutumika kwenye maisha ya kawaida, majaji wa mashindano hayo wanasema kifaa hicho kitaboresha elimu mashuleni kwa walemavu(vipofu na viziwi) kwasababu kinaweza kikatumika kufunza pia, sanasana kwenye hesabu.
 
esther_amimo_and_salome_njeri_at_the_international_science_and_engineering_fairisef_0.jpg
Sana. Hawa wanafunzi ni wabunifu kupindukia na wameiwakilisha nchi yao ya Kenya vilivyo. International Science and Engineering Fair(ISEF) ni mashindano ya kimataifa ya kisayansi yanayowashirikisha wanafunzi 1,800 kutoka nchi 75 duniani! Wadhamini wa mashindano hayo ya kila mwaka ni U.N., kupitia shirika lao la U.N. Science and Cultural Organisation na ndio mashindano makubwa kabisa ya kisayansi kwa wanafunzi wa shule za upili duniani. Hiki kifaa chao 'Essameter' ambacho jina lake limeunganisha majina yao Esther na Salome ndio walishinda nacho kwenye 56th Kenya National Science & Engineering Fair 2019. Wakenya waliofuzu kwa mashindano hayo ya kimataifa yaliyokuwa kule U.S.A mwaka huu ni wanafunzi kumi kutoka shule tatu nchini.
Kenyans are very ambitious at a personal level.That has what has kept us going even when every odd is against us.
We will go even further if we get support for science and technology innovations.
 
Back
Top Bottom