Wanafunzi wawili wa kike kutoka Shule ya Msingi ya Kenana, eneo la Njoro Kaunti ya Nakuru, wamekosa masomo kwa wiki moja wakidai kudhalilishwa na kuadhibiwa na mwalimu wa kike kwa kosa la kutovaa nguo za ndani. Tukio hilo limeripotiwa kuwatia hofu na kuwafanya wasisite kurudi shuleni.
Kwa mujibu wa madai yao, mwalimu huyo alimlazimisha mmoja wa wanafunzi kuvua suruali aliyokuwa amevaa chini ya sare ya shule, kisha akampiga. Baada ya hapo, alimburuta hadi chumba cha walimu na kumtangaza mbele ya walimu wengine zaidi ya 20 kwamba hakuwa amevaa nguo ya ndani
Madai hayo pia yanahusisha dada yake, ambaye naye alipitia udhalilishaji sawa. Hali hiyo imewaacha watoto hao wakiwa na mshtuko wa kisaikolojia na hofu kubwa ya kurudi darasani kutokana na aibu na mzaha waliofanyiwa mbele ya wenzao na walimu.
--------------------
------------------
Two sisters from Kenana Primary School in Njoro, Nakuru County, have missed classes for a week after allegedly facing humiliation and punishment from a female teacher over not wearing inner garments
The siblings claim the teacher forced one of them to remove a trouser worn under her school uniform before subjecting her to punishment. She is said to have then dragged the learner to the staffroom, where, in the presence of about 20 other teachers, she announced that the pupil was not wearing panties
The same treatment was reportedly extended to the second sister, leaving both children distressed. The learners now say they fear returning to school due to the ridicule and embarrassment they endured