Wanafunzi wenye vipaji maalum!!!

Sio mbaya !

Natoa ushuhuda.

Nimesoma kibaha na sasa nasoma MD abroad.

Wanafunzi toka Kibaha hapa ni 7 sasa.Maprof wamewatukubali.Tupo kwenye vyuo 3 ,lakin kwa kila chuo maprof wameshaonesha apreciation.
Ni vizuri kujenga mazoea ya appreciation maana duniani tuna uwezo tofauti ,tumejaliwa viwango tofauti vya kufikiria.
Tanzania yetu haiwapi wenye vipaji nafasi kuonesha vipaji vyao,mfano kuna Mtanzania Hungari ni Engeneer mzuri sana na wizara ya elimu walimfuata wakashindwana kwenye malipo ,hela zote EPA,TANGOLD ,KAGODA n.k,

TUIBADILISHE SERIKALI.
 

Kweli kabisa, sijui hata wako wapi manake walikuwa na mbwembwe hao acha tu
 
Lazima tukubali kuwa vipaji vinatofautiana toka mtu hadi mtu. Kuna wenye vipaji zaidi kuliko wengine. Kwa mfumo uliokuwepo na ambao upo mpaka sasa, kipaji kinapimwa kwa kuangalia ufaulu wa mwanafunzi toka shule ya msingi kwenda sekondari. Hiki mimi bado naamini ni kigezo kizuri cha kutofautisha watu wenye kipaji na wale wasiokuwa na kipaji. Kinachotakiwa ni kuboresha mfumo wa kuwatambua na kuwaendeleza wenye vipaji ili waweze kuwa chachu ya maendeleo nchini. Mfano, mitaala ya shule zao ingeongeza mafunzo ya kutafiti/kugundua vitu vipya vitakavyosaidia kutatua matatizo katika jamii zinazowazunguka badala ya kuwekeza kwenye kufaulu mitihani peke yake. Wenzetu wanaita ingenuity. Lakini pia unapokuwa na mwanafunzi mwenye kipaji unahitaji kuwa na mwalimu mwenye kipaji aliyefunzwa vizuri kulea na kuendeleza kipaji cha huyo mwanafunzi.
 

vipaji maalumu ndiyo nini?
 
ni kweli bwana mkubwa ,shida ya nchi yetu ni kwamba watu wanamaliza vyuo bado wanafanya research za kuibia. Msitegemee wanafaunzi special wakaleta moto toka mbinguni ,haiwezekani . Lakini nasikitika hawa akina Karamagi ,Mkuu mwenyewe akina Mgonjwa alumni wa Kibaha shule ya wizara wameonesha negative force to our development.
 
Tatizo kubwa ni kutowapa nafasi,bila utafiti hakuna haja ya kuponda maana wanaopinga watoe utafiti wenye kushikika
 
oh !men i like this debate,okengineer anasifika kwa kusoma mahesab kila anapopekua kurasa za kitab chake,tusiende mbali,tujiulize ni wangapi wanaoelewa hesab na kujua kuiapply?
 

Gamba la Nyoka.UMENIKUNA SANA MTU WNG ni hivi hao wanajiita vipaji maalumu tulikuwa tunakutana nao Don Bosco ila cha kushangaza hawana mchango wa maana kwenye Disc.Nachokumbuka ni kuwa mi nilikuwa na rafiki yangu alikuwa anasoma shule ya msing Majohe" na nilimpita marks 9.ila matokeo yake yeye akachaguliwa Mzumbe kisa Majohe inajulikana kuwa ni Ilala vijijin niliumia ila skul yangu ilikuwa Ukonga.Cha ajabu akirudi mi ndo mwalimu wake.CHA MSING NI KUWA kipaji maalumu hajulikani kwa last examination tuu ndio maana weng wao Hawana mchango kwenye jamii na hata kudisco .Azania wengi wao ndo wanafunzi ambao walikuwa wanaburuza kwenye primary za Dar.
 

achana na mambo ya kuchana wewe bwa mdogo fikiria hyo A yako unayoipata itakuwa na maslah gani kwa taifa? Bora hata tumthamini mtu anaye pata D lakini anajua kulitetea taifa.
 
Uspecial una maana pale unapotumika bt othwise Special School are similar to Kata School..and this is whats going on in our Country
 
Special guys wako oxford,havard na princeton..sio bongo.
 
achana na mambo ya kuchana wewe bwa mdogo fikiria hyo A yako unayoipata itakuwa na maslah gani kwa taifa? Bora hata tumthamini mtu anaye pata D lakini anajua kulitetea taifa.

Haya dogo nimekusoma ila tupo at the same side chunguza vizuri conclusion yangu.
 
Kataa usikatae kuna average students na exceptional students. Na wengi wetu ni average students Hilo lipo na litaendelea kuwapo. Kwamba hao exceptional students wamelifanyia nini taifa ni suala la sera. Kama sera za taifa hazitoi nafasi ya kuwaendeleza na kuwasaidia katika tafiti na uvumbuzi mchango wao hatutaufaidi kama taifa bali familia zao tu (kwa vipato wapatvyo toka katika ajira zao).
 

Nani huunda hizo sera bora? Au hudondoshwa toka mbinguni na mungu?
 

Hujawahi kukutana na mwanafunzi mwenye kipaji wewe. Vinginevyo mtazamo wako usingekua huu.
 
Hao waliokasimishwa hayo mamlaka wamekasimishwa na nani? Mungu?

Ni sisi wenyewe ndio tuliowakasimisha. Mkuu naomba nikutangizie sijui kama ntakua nadandia gari kwa mbele. Wa kulaumiwa ni sisi wananchi wenye mamlaka ya kuwakasimisha watu flani kama watunga sera wetu halafu hapahapa kwa matokeo ya sera mbovu zilizopo tunaanza kuulizana wako wapi/ uko wapi mchango wa wanafunzi wa vipaji maalumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…