Hayo ni matokeo ya wanasiasa ku-dominate katika elimu. Kwa maoni yangu, ninaona viboko bado vinatakiwa kwa mazingira ya wanafunziu wetu wa Tanzania. Niinaamini, mashirika mengi yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayoshughulika na elimu(ikiwa ni pamoja na kukampeni matumizi ya viboko yasitishwe na zitumike adhabu mbadala) yanaendeshwa kwa miongozo ya wafadhili wao wa nje ambao mazingira ya kwao(namna ya maisha kwa ujumla) ni tofauti kabisa na kwetu. Watawala wetu(wanasiasa) wamekuwa wakipokea kila maelekezo kutoka kwa wafadhili bila kujali kama yana-apply au haya-apply kwenye mazingira yetu. Cha msingi mimi ninachoona ni kwamba viboko bado vina tija kwa mazingira yetu cha msingi walimu kuelekezwa namna na maeneo salama ya kumchapa mwanafunzi , pia kuepuka matumizi ya adhabu hii mwalimu anapokuwa na hasira ili kuepuka madhara . Mimi ninaposoma nilikuwa nikiogopa sana makora na nilipenda adhabu za nje.Pia adhabu za nje ni adhabu kwa mwalimu pia kwani atatakiwa kusimamia kuhakikisha adhabu husika inakamilishwa katika mazingira salama kwa mwanafunzi.