Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Tukio la kikatili limeripotiwa kutokea Septemba 7, 2022 majira ya asubuhi Shule ya Sekondari Songwe, Kata ya Bonde la Songwe kwa wanafunzi wa kidato cha pili na cha nne waliopo shuleni hapo kwa maandalizi ya mitihani ya Taifa.
Inadaiwa kuwa walimu wa shule hiyo ambao kwa majina ni Lugongo, Kasambala, Jengela na Geazi walikuta kinyesi cha binadamu kwenye mojawapo ya madarasa ya shule. Baada ya wanafunzi wote kuulizwa na kukana kufanya kitendo hicho, walimu hao waliamuru wanafunzi wajipange mstari kwa lazima, kisha kuwalazimisha kila mmoja kushika kinyesi kile kwa mikono kama sehemu ya adhabu.
Wanafunzi walio kataa kufanya kitendo hiki walikuwa wanapigwa hadi wakubali, na walimu hao walitoa onyo kali kuwa ikitokea siku nyingine kitendo kama hiki kitatokea tena, siku hiyo wote hawatalala na kinyesi hicho kitapakwa usoni kwa kila mmoja wao kama mafuta.
=============
Baadhi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Songwe ya Kata ya Bonde la Songwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini wanatuhumiwa kuwalazimisha Wanafunzi zaidi ya 100 wa kidato cha pili na nne kushika kinyesi cha binadamu kama sehemu ya adhabu.
Walimu walitoa agizo hilo baada ya kukuta kinyesi darasani, baada ya kuwahoji wakawapangisha mstari na kuanza kuwalazimisha washike, aliyekataa alichapwa hadi kukubali.
Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya, Ernest Hinju amesema alijulishwa juu ya tukio hilo na hatua zilitakiwa kuchukuliwa kwa Walimu waliohusika. Amesema “Nipo nje ya ofisi, nitafuatilia majibu ya hatua zilizochukuliwa kisha nitatoa taarifa.”