voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,935
Mmekuwa mkiililia serikali hususan awamu ya tano, iliyopita.
Kwamba ilikandamiza na kuuminya Uhuru wa kuongea na kutoa maoni nchini. Ikiwemo kuminya Uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania. Sasa ni awamu ya sita chini ya Samia Suluhu Hassan. Ameifungua nchi kimataifa.
Pia amewapa Uhuru wenu pamoja na kuwarudishia waziri wenu mpendwa. Kwenye wizara ile ile mliyokuwa nae mkiulilia Uhuru pamoja. Amekutana na nyinyi na mmewekeana "MOU"
Lakini tukiangalia Kwenye Media Press nchini na kinachoendelea kwa sasa hatuoni tofauti kivitendo. Mambo ni yaleyale kama ilivyokuwa huko tulikotoka. Mlipaswa kuelewa jinsi ya kufanya kazi ya uanahabari katika kipindi hiki. Ili kwenda sambamba na ukuaji mkubwa tena wa kasi waTeknolojia ya mawasiliano Duniani.
Sasa hivi kwa asilimia kubwa Duniani na Tanzania ikiwemo. Watu wengi ni rahisi kujua ni nini kinaendelea popote pale Duniani kutokana na uwepo wa teknolojia ya Simu janja zao. Na inakuwa ni rahisi mtu yeyote kuripoti habari ya tukio kutokea saa hiyo hiyo linapotokea. Kabla hata halijafika kwenye vyombo vya habari.mfano kupitia humu JamiiForums
Waandishi wa habari wa nchi hii. Ili kuiokoa sekta yenu isijifie taratibu kama tunavyoonabikizidi kudorola kwa sasa. Mfano
Kupitia soko linaloyumba la magazeti huko mitaani. Mnapaswa kuacha kulialia sambamba na wanasiasa badala yake mwende mbele zaidi kiuandishi na utafiti wa habari.
Mbadili mfumo wenu wa utendaji kazi.muache mtindo wa kuishia kuripoti matukio na kuishia hapo. Mwende far beyond na kuleta habari za uchunguzi na zenye weledi wa kina sababu nyinyi mmesomea kazi hiyo. Tofauti na sisi tunaoishia kuripoti kile ambacho macho yetu yameona.
Mje na habari zenye muendelezo wa matukio kwa kina na zenye kuihabarisha na kuielimisha jamii yetu. Pale mnapopata nafasi za kufanya mahojiano na viongozi waandamizi nchini.
Wawe wa kiserikali au kisiasa, msiishie kujipendekeza kwa kutanguliza uheshimiwa wao mbele. Bali muuweke pembeni na
muuvae uanahabari wenye weledi kwa kuuliza maswali yenye tija na yanayoihusu na kuigusa jamii kuhusiana na mada husika itakayokuwa mezani. Tena kwa weledi zaidi. Jaribuni kuiga wenzenu wa mashirika ya nje.
Badala ya kushinda mkitafuta udaku na press release zenye kuandamana na bahasha zenye posho. Kisha mkaishia kutuletea habari zilizolalia upande wa watoa Bahasha wazuri. Mwende kwenye jamii huko ndani na kutuletea habari halisi zenye jicho la mwanahabari msomi. Pia muwe mnafanya muendelezo wake.
Mfano!
mliandika na kuripoti tukio la vijana watano waliopotea katika mazingira tata jijini Dar es Salaam mwezi wa December 26/2021.
Baadae hakuna mrejesho wa kilichoendelea mpaka sasa. Ingawa sakata hilo halijapatiwa ufumbuzi mpaka sasa.
Lakini Media zetu hakuna hata moja ambayo imechukua one step ahead na kurudi kwenye zile familia, au kurudi kwenye vyombo husika ili kuwajulisha wananchi na hivyo kuwaondolea taharuki husika kwa kupata mrejesho.
Badala yake mko kawaida mkiendelea kutuletea habari fupifupi tena zingine zenye lugha za kihuni kwa jamii kama. Akinukisha.
Kimenuka hiko kitu. Balaa jingine...
Na mara nyingi maudhui ya habari hayaakisi au kuendana na vichwa vya habari husika.
Nawauliza wanahabari mnakwama wapi?
commonmwananchi
10101