Hivi karibuni Mbunge wetu wa Iramba Magharibi na Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Lameck Nchemba alikuja kujiandikisha kwenye Daftari la Kupiga Kura kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Misigiri kilichopo Kata ya Ulemo wilayani Iramba, Mkoani Singida.
Baada ya kujiandikisha wananchi tuliokusanyika pale tulitoa malalamiko yetu juu ya changamoto mbalimbali ambazo Mbunge wetu hajatatua. Vyombo vya habari vilikuwepo pale tulizungumza kwa uchungu juu ya huyu mbunge wetu ambaye ametusahau kimaendeleo.
Cha kusikitisha HAKUNA MWANAHABARI HATA MMOJA ALIYETOA MALALAMIKO YETU KWENYE VYOMBO VYA HABARI. Habari iliyotoka ni ya mbunge kujiandikisha tu kana kwamba hakuna lingine lililotokea.
Kwa hali hii tutakuwa na uhakika gani wa taarifa zitakazo kuwa zinatolewa kwetu? Hadi sasa tunaamini kuwa wanachotaka wanasiasa ndicho kinacholetwa kwetu na sio uhalisia wa yanayotokea.
INASIKITISHA SANA.
============== ========================