informer 06
Member
- May 11, 2024
- 66
- 49
Mamlaka ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesewahasa waandishi wa habari za Mtandaoni (digital online) kuhamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kudai risiti pale wanapofanya manunuzi ili kusaidia Serikali isikose mapato.
𝖯𝗂𝖼𝗁𝖺𝗇𝗂 ; Hudson Kamoga
Rai hiyo ameitoa leo Jijini Dar es salaam, Mei 29,2024 na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mapato TRA Elimu ya elimu ya mlipa kodi na Mawasiliano kwa Umma, Hudson Kamoga katika Semina iliyoandaluwa Jukwaa la Waandishi wa habari wa Mtandaoni (JUMIKITA) kwa kushirikiana na TRA ambapo amesema waandishi hawana budi kuwa wazalendo na Taifa lao kuweza kusaidia katika mchakato mzima wa ukusanyaji mapato kulingana na taratibu.
“Tunatambua kuwa dunia imekuwa kijiji kwa ajili ya Mitandao ya kijamii hivyo kundi hili la waandishi wa habari wa mtandao watatusaidia sanaa kwani kuna wafanyabiashara wengi wanafanyabishara kidigital kupitia semina hii italeta tija kwa Wananchi kukusanya mapato huko walipo na kuwajengea utamaduni wa kulipa kodi kidigitali bila usumbufu wowote” amesema Kamoga
Pia ameongoza Serikali ilikuja na utaratibu mpya wa kukusanya kodi kwa baadhi ya wadau wanaopata pesa kwa watanzania licha ya kutokuwa na ofisi nchini, amedai kuwa utaratibu huo ulikuja baada ya kugundua uwepo wa baadhi ya wafanyabishara ambapo hawana ukaazi Tanzania lakini shughuli zao hutumia mitandao ya kijamii kukutana na wateja wao.
Hivyo amesema kuwa Semina hiyo kupitia wanahabari inasaidia kuwaongezea uelewa ambao utasaidia kuwafikishia taarifa na kuelewa taratibu mbalimbali kuhusu suala hilo pamoja na mengine.
Kuhusu utaratibu huo mgeni wa kikodi amesema kuwa umechangia ongezeko la mapato tokea ulipoanzishwa, ambapo amesema kuwa kwa takwimu zisizo rasmi kulingana na taarifa ya mwisho aliyokuwa nayo kwamba mpaka wakati anazungumza Bilioni zaidi ya 11 zilikuwa zimekusanywa kwa mwaka wa fedha unaoelekea kuhitimishwa ikiwa ni ongezeko la asilimia zaidi ya asilimia 60 kutoka utaratibu huo ulipo anzishwa, ambapo hicho kikiwa kipindi cha pili.
𝖯𝗂𝖼𝗁𝖺𝗇𝗂 ;Shabani Matwebe
Aidha kwa upande wa Mwenyekiti wa JUMIKITA, Shabani Matwebe ameshukuru sanaa TRA kutambua mchango wa wanahabari wa mtandaoni kwa kuwapatia semina adhimu kwa mara ya kwanza, ambapo alidai kuwa semina hiyo italeta tija kwenye mchakato mzima wa ukusanyaji mapato kupitia ujuzi watakaoupata wanahabari na kuufikisha kwa umma.
Semina hiyo ilikutanisha wanahabari zaidi ya 100 kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambayo haswa utumia mitandao kufikisha maudhui kwa umma.