Wanaharakati kuweni wazalendo, baadhi yao ni waongo sana na wanapotosha kuhusu katiba pendekezwa

Wanaharakati kuweni wazalendo, baadhi yao ni waongo sana na wanapotosha kuhusu katiba pendekezwa

Joined
Mar 7, 2015
Posts
21
Reaction score
1
Kuna hoja kwamba haki za binadamu hazina ulinzi wala hifadhi ya kikatiba ndani ya katiba inayopendekezwa.
Kauli hii ni yauongo na haifai kuendelezwa kuwadanganya watu.
ibara ya 64(1) ya katiba pendekezwa inasema hivi,serikali na mamlaka ya nchi ina wajibu wa kuzingatia na kuhifadhi haki za binadamu ikiwa ni msingi wa uhuru kama ilivyoainishwa katika katiba hii.

ibara ndogo (2) inasema, haki na uhuru wa kila mtu kama ilivyoainishwa katika katiba hii utaheshimiwa, kuhifadhiwa na kudumishwa na mamlaka ya nchi, taasisi binafsi na kila mwananchi.

Ibara ya 65 ni mahususi kwa usimamizi wa haki za binadamu, ibara ndogo (1) inasema hivi, katika kutafsiri mashariti ya sura hii ya haki za binadamu, mahakama au chombo kingine chochote cha kufanya uamuzi kitazingatian mambo yafuatayo: (a) sheria za kimataifa na haki za binadamu, na (b) haki za jamii na maslahi ya jamii kwa ujumla.

Ibara ya 65(2) inasema hivi, mtu anayeamini kuwa mashariti yaliyomo katika sura hii ( yaani sura ya haki za binadamu) yamekiukwa au yanaelekea kukiukwa na mamlaka, chombo cha uamuzi, sheria au sera yoyote dhidi yake, anaweza kufungua shauri katika mahakama kuu kwa hati maalum ya maombi kwa mujibu wa sheria za nchi ili kupata nafuu inayohitajika.

Ibara ya 65(5) inasema hivi, endapo katika shauri lolote inadaiwa kwamba sheria yoyote iliyotungwa au hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali au mamlaka nyingine inafuta au inakataza haki, uhuru na wajibu muhimun utakaotokana na ibara ya 32-59, (ambazo ni ibara za haki za binadamu) na mahakama kuu kama inaridhika basi itatoa tamko kwamba sheria au hatua inayohusika ni batili au kinyume cha katiba.

Ibara ya 65(6) inatoa uhuru kwa mahakama kuu iwapo kutakuwa na sheria yoyote inayokiuka haki za binadamu, mahakama kuu itakuwa na uwezo wa kuamua au kutoa fursa kwa mamlaka nyingine yoyote inayohusika kurekebisha sheria hiyo na mamlaka hiyo itapewa na muda na mahakama wa kufanya marekebisho hayo na iwapo muda uliotolewa na mahakamakuu utakwisha kabla ya mamlaka hiyo kurekebisha hitilafu hiyo basi itakuwa ni halali kwa mahakama kutoitumia sheria hiyo.

UKO WAPI UKWELI WA KAULI YA KWAMBA KATIBA INAYOPENDEKEZWA HAIJALINDA HAKI ZA BINADAMU? KAMA HAMNA HOJA ZA KUWAELIMISHA WATU KUHUSU KATIBA KWA NINI MSIKAE KIMYA? AU NDO FEDHA ZA WAFADHILI ZINAWATOA UZALENDO NA KUAMUA KUWA WASALITI WA NCHI YENU KWA KUTOTENDA HAKI JUU YA TAIFA LENU?

MSITUMIE ELIMU ZENU VIBAYA KWA KUANGALIA NJAA ZENU, HILI NI TAIFA LETU SOTE, KUWENI WAADILIFU ILI WATU WAELEWE NINI CHA KUFANYA KUHUSU KATIBA INAYOPENDEKEZWA.

NI MWANASHERIA,
MWESIGWA ZAIDI SIRAJI.
0784 646220
 
Vile umeipuuza rasimu ya warioba basi watu hapa pia watakupuuza.
 
Back
Top Bottom