VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Zikisalia siku chache kufunguliwa kwa Vyuo Vikuu nchini,Wanafunzi Wanaharakati Vyuoni wamesema kuwa migomo haiepukiki. Wakizungumza nami katika nyakati tofautitofauti,wanaharakati hao wameapa kuwa vyuoni patachimbika. 'Kwa ubaguzi huu wa kozi fulani kupewa mikopo na nyingine kunyimwa,Vyuoni hapatakuwa sehemu salama kuishi' wametamba. 'Hatutakubali ubaguzi kwenye nchi yetu wenyewe' wakaongeza.
Serikali na isikie...
Kalaga baho...Mkuu, Vyuoni siku hizi kuna wanaharakati?! Tangu lini? Una uhakika ni vyuo vyote? Waliyasema hayo wapi? Wakiongea na wewe kama nani? ..Una uhakika kuwa si mawazo yako na ku-generalize kwamba hao "wanaharakati" wanasema hivyo? Source ya info?
Aiseee wangoje 2malize mwaka 3 ndio waanze hizo harakati
Mbona umesahau kuweka Aiseee Babaangu. . . . .