Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
Hivi Shekhe Farid Hadi Ahmed na wenzake wameshitakiwa kwa kosa la uhaini au ugaidi au mauaji ndio maana hata sasa wako rumande? Mwenye kujua anijulishe. Hivi watetea haki za kibinadamu wa Tanzania hawajui kuwa watu hawa nao ni binadamu? Hawajui kuwa mambo wanayofanyiwa ni kinyume cha haki za binadamu? Wanashindwa kuwatetea kisa tu watu hawa ni UAMSHO? Hawataki kuwatetea kwa kuchelea kukosa misaada kutoka magharibi? au?
Hata vyombo vyetu vya habari haviripoti madhira yanayowakumba hawa watu, na hata vikizungumza, vinazungumza katika namna ya kuwahusisha na ugaidi kama vile kila muislamu anayefanya harakati za kupigania stahili zake na kufuga ndefu ni gaidi. Wale ni wanzibar na si magaidi, na katika historia ya nchi yetu kila mzanzibar mipigania mamlaka kamili ya Zanzibar hupatwa na misukosuko, kuuawa na kuzushia kila aina la chafu.
Wengi wamepotea katika mazingira tatanishi, wengi wamepotezwa kisiasa na wengi wamenyamazishwa na kutulizwa kama maji ya mtungi. Seif Sharifu, Hamad Rashid, Abdul Jumbe, Abeid Karume, nk. Tusitumie nguvu haramu kuulinda muungano, bali tutumie nguvu ya kisheria inayozingatia udugu na upendo. Hawa watu hawana watetezi huenda kutokana na uislamu wao na misimamo yao[hii ni dhana].
Sijui Wazanzibari na Watanzania wenzangu kwa ujumla tunapofuturu na aila zetu katika mwezi huu mtukufu kama tunawafikiria wananchi wenzetu walio gerezani kwa makosa ya kupika na kutengenezwa yenye lango la kuulinda muungano, bila kujua kwa kufanya hivyo[hiyo serikali] ndio kwanza wanauchimbia kaburi muungano.
Nasema ni makosa ya kupika kwasababu zile vurugu zote za Zanzibar za uchomaji moto makanisa na zinginezo zimefanywa na kidudumtu mwenye lengo la kuleta fitna kati ya UAMSHO na umma wa kizanzibar, lakini kubwa ni kuwatafutia kesi wanaharakati hawa ili kuzorotesha kazi zinazofanywa na UAMSHO ambazo wazanzibar pasina kuzingatia tafauti zao za kisiasa wamezikubali kazi hizo. Kesi za kubambikia kwa wanaharaki imeshakuwa mtindo wa kisasa nchini petu, sijui tumeuiga wapi?
Wazanzibar wako na sababu nyingi sana za kulinda makanisa na mali zake lakini hawana sababu hata moja ya kuchoma makanisa na kuharibu mali za makanisa. Nasema hapa kuna kidudumtu, litakuwa jambo jema endapo wazanzibar watamjua huyo kidudumtu kabla hata ya kura za maoni kwa rasimu ya katiba na uchaguzi mkuu ujao.
"Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nymba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu" quran 40:22
Pamoja na mambo mengine aya hiyo inamrisha waislamu wasivunje na kuharibu nyumba za ibada za dini zingine, huwezi kushika kiberiti na kuchoma kanisa na bado ukajiita muislamu wakati wafanya kitendo hicho ilihali wavunja amri ya M/mungu. Hivi Shekhe Mselem haijui hii aya? Viwanja vilivyojengwa makanisa vimetolewa na waislamu wenyewe, sasa iweje waislamu wenyewe wahusike katika kuyaharibu makanisa? Alafu, kwanini makanisa siku zote yako salama, lakini watu walipoanza kudai Zanzibar yenye mamlaka kamili ndio makanisa yaanze kuchomwa moto? Hivi tukisema lengo ni kupoteza upepo wa mijadala ya amani iliyokuwa ikiendeshwa na UAMSHO tutakosea?
"Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui. " quran 2:190
Pamoja na mafunzo mengine, aya hiyo inamkataza muislamu kuzua ugomvi, kujitegeza na kuanzisha vita. Ili mislamu aingie vitani au kupigana shuruti achokozwe, tena uchokozi wenye kutishia usalama waislamu na binadamu wasio na hatia hata kama si waislamu. Ni lini wakristo wa Zanzibar waliwachokoza waislamu? Lini wakristo wa Zanzibar walichoma misikiti? Kwakuwa Wakristo hawakuwahi kufanya jambo lolote baya dhidi ya waislamu, hivyo basi waislamu hawana sababu ya kuwashukia wakristo. Tusipotoshe na wala tusipoteshwe, mgogoro uliopo ni kati ya dola na waislamu na kwa yeyote mwenye azima ya kuwatumia wakristo katika jitihada za kuzima harakati za waislamu huyo ni wa kuogopwa kama "ukoma", kwani kufanikiwa kwake hakutaaiacha nchi yetu salama.
Binafsi mimi ni muumini wa serikali MOJA, na si serikali tatu wala mbili, hivyo harakati za UAMSHO SIZIPENDI, ila na wao harakati zangu hawazipendi, tujenge hoja na tuziuze kwa umma, wenyewe umma ndio utaamua nani mshindi na si vitendo vibaya wanavyofanyiwa wenzetu. Wakati tukifuturu tuwakumbuke na waislamu wenzetu walio gerezani kwa kosa la kutishia ulaji wa wahafidhina wa CCM na wanafiki wa CUF.[Ipo siku nitafafanua].
Farid Hadi Ahmed,
Msellem Ali Msellem,
Mussa Juma Issa,
Azan Khalid Hamdani,
Suleiman Juma Suleiman,
Khamis Ali Suleiman,
Hassan Bakari Suleiman,
Ghalib Ahmada Omar,
Abdalla Said Ali,
Fikirini Majaliwa Fikirini.
IJUMAA KAREEM.
Njano5.
0784845394.