WanaHipHop wote tukutane hapa Fid q Vs Nash Emcee (2)

Kitabu chako binafsi naona hakina tija kabisa kwa jamii nzima ya vichwa wa Hip Hop. Sikukatishi tamaa, la hasha! Maudhui ya kitabu chako hayawezi kuamsha hisia za ndani, itikadi na imani kwa wachemkaji ama wale wanaojinasibu kuwa wanajamii ya Hip Hop. Hisia zako ndugu mwandishi zinaongozwa zaidi na mihemko ya hapa na pale pamoja na matukio flani flani yaliyotokea punde kuhusiana na fani ya hapa nyumbani Bongo. Nasema tena maudhui hayana mashiko ya kuitwa kitabu cha Hip Hop. Makusanyo ya mtandaoni na kutoka mitandao ya kijamii ndio muongozo wako hasa. Ingekuwa rahisi namna hii, kungekuwepo na hazina kubwa sana ya kutosha ya hivi vitabu. Binafsi sikufahamu wewe na ada/mchango wako uliolipa/unaolipa katika hii fani hivyo inaweka ukungu sana katika taswira ninayotazama toka kwako na hiki kitabu. Nilitazama mada zote za hiki kitabu, binafsi hakuna jipya la kuingiza zaidi ya tungeketi wana kadhaa kisha tukaanza kusimuliana haya yote na kupeana tano, kisha tusikikize ngoma kadhaa tutawanyike. Sina chuki, wivu au majungu. Naheshimu muda na nguvu pamoja na akili unazotumia kuandaa hii kitu. Baadhi ya jamii zimepinga sana juhudi zako za kuandaa kitabu cha Hip Hop hapa Bongo kikiwa na maudhui mepesi namna hiyo. Fuatilia namna Gospel Of Hip Hop kilivoandaliwa, The Tao of Wu cha RZA, There Is A God On The Mic cha Kool Moe Dee, How To Rap(part 1&2) pamoja na makala kibao zakina Davey D na vichwa wengine wanaotunza historia adhimu ya huu Utamaduni wa Hip Hop na watu wake kwa ujumla. Mfano simulizi za mahusiano/majibizano ya huyo Fid Q na Nash, ningeweza kufuatilia huko mtandaoni na vijiweni kote wanakokaa ama kuzungumziwa hawa watu. Hip Hop ni zaidi ya hao vichwa wawili ndugu. Kuna mengi ya dhati kuyaandika zaidi ya hayo kuhusiana na fani yetu hapa nyumbani. Kurasa zinazosherehesha suala la hawa wandugu ni uchafu katika kitabu chako. Kama wanawania kuwa kinara kwa mtindo huo, hawajengi fani. Bado nafunguka... Kuna mada za kina Assata Shakur na kina Jadakiss wa The Lox, kaka, kitabu si kirahisi namna hii. Kama kuna wana wamekupa gwara kuandaa hii kitu, sio mbaya, ila kuandaa kitabu hasa cha Hip Hop, au makala, ni kitu ingine. Sema kishkaji shkaji tu zile za maskani mbona hapo umetishaaaa sana kaka. Hakuna kitu rahisi ndani ya Hip Hop. Hata kimoja. Hii inatokana na kuwa mtindo wa maisha wa watu flani flani. Watu hao wanaamini katika namna mbali mbali ndani ya hiyo Hip Hop. Machafuko ni mengi. Amani hutoweka muda mwingi na kurejeshwa kwa namna kadhaa kama vile kufanya ngoma/onesho kwa pamoja kutembeleana maskani na kuwa na Session za pamoja..namna hiyo. Watu wote waliotofautiana kunako Hip Hop wanatakiwa warejeane kwa pamoja na kufuta tofauti zao na kushirikiana katika kujenga fani hii kwa pamoja. Na sio majibizano katika mitandao ya kijamii tu huku uchechezi ukizidi kutoka kwa watu wao wanaowakubali.
 
Ni angalau ulichokianfika kinaweza kuuzika, kwa sababu umejitahidi kutumia upeo wako kuchambua jambo, sio mtu anatoa tweet mtandaoni alafu anaandika kitabu.
 
NASH MC MZUZU MAALIM



MASWALI YA KIWAKI

MKONGWE

MITIHANI

TABIA

SHUJAA

nk hyu mtu ni hatare sana aiseeh... msikikizeni
 
Nahisi kuna mmoja hapo ana inferiority complex
 
Unafananisha sauti ya ushuzi na sauti ya radi, fid q mashine nyingine.
 
Et Fid na Chindo haziivi? sasa walifanyaje ile torati ya mtaa? Tatizo la Nash anajifanyaga HIPHOP Anaijua yeye peke yake na Nguzo zote anazo yeye tu. hilo ndo tatizo lake tuu akifanikiwa kuachana na upuuzi huo huenda akawa mwanahiphop mzuri tu.
Sijawahi kujua huyo Nash kama kuna msanii wa hiphop anamkubali hapa bongo, maana anajikuta yeye tu ndio anafanya hiphop. By the way Nash huwezi mfananisha na FID hata kidogo, Nash yuko kawaida sana
 
Kuna wanakufofoka watano tu nchi hii,,fid,joh makin,roma,mwana fa,afande selle,,wengine ni wakal pia ila vichwa ndio hvyo hapo. Km haupo hapo waambie wakaze buti
Toa joh ...Nikki mbishi songa one incredible
 
Acha kumfananisha Fid q na vitu vya kipuuzi.
Baada ya hizo tweets na mistari ya huyo Nash, Je Fid alishawahi kujibu chochote..?
 
ni upumbavu kabisa huu nach mc level zake ni kina kemical cyo fid Q
 
Hiphop inajibiwa kwa nyimbo...huwezi msifia msanii kwa ku tweet..toa reference ya nyimbo zake...album ngap...nyimbo zake kali ni zipi...hivi ndo vigezo vya msanii...sio kukaa kwny computer ku tweet hizo mambo wanafanya wakina trump daily
 
Nash ni mpuuzi kuna siku nikaskia anasema Nash EMCEE Uandishi kama wa shaban robert nikasema huyu mpuuzi hana anachokijua zaidi ya kufuga mandevu uchizi tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…