pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Biashara za wasauz kule Nigeria zimepata pigo la hasara na uharibifu wa mali baada ya wanigeria wenye hamaki kufanya uvamizi. Supermarket za Shoprite na mali za MTN kwenye miji kama Lekki, Lagos na pia Ogun State zimevamiwa na mali ya hela nyingi kuibiwa na kuharibiwa. Huu ni muendelezo wa vurugu zinazoendelea A.K. dhidi ya wageni kutoka nchi mbali mbali za Afrika. Ambapo wanigeria kule A.K. ndio walioathirika zaidi. Lets all say NO to Xenophobia. Haina faida kabisa zaidi ya hasara na aibu kwa bara hili letu la Afrika.