Lyambalyetu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2021
- 278
- 255
Baada ya kuwa Mwanza kwa takriban miezi mitatu, juma lililopita nikarejea na kuamua kukusanya ndengu Jimbo la Iramba na hivyo kunilazimu kutembelea vijiji ambavyo wanalima ndengu.
Ndengu ni mojawapo ya zao tunalolima sana Iramba, ukiacha alzeti na zamani vitunguu.
Katika pitapita zangu huko na kuulizia wajihi na umuhimu wa Mbunge wetu wa sasa Dr. Mwigulu. Kwa sasa anatajwa kwa kutokuwa na tabia ya ukarimu kama watangulizi wake akina Shango na Kiula.
Juma Kilimba amabye kwa sasa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa alikuwa ni mtaalamu wa kuhonga lakini hakuwa mkarimu na ndiyo maana ilipofika 2010 alishindwa kiurahis sana na Dk. Mwigulu.
WanaIramba wanadai Mzee Shango alikuwa akiwakuta kwenye klabu anakaa nao na anawanunulia pombe yote pale kwenye Klabu wanainywa wanafurahi na wanaendelea na maisha yao.
Shango na Mzee kiula ndiyo tabia zao zilikuwa zinalandana ingawa Shango alikuwa mkarimu kwa watu wa namna zote.
Upande wa Mwigulu wanadai anajidai sana. Akifika msibani anabaki kwenye gari mpaka aongozwe kushuka na Mlinzi/Msaidizi wake. Kula hivyo hivyo mpaka Mlinzi wake atangulie kula ndiyo naye ale.
Dkt. Mwigulu hatoi fedha kiholela na inaonesha anadaharau sana maisha yao - wakiwa wanakunywa pombe Klabuni anapita tu na ligari lake na kuna wakati aliwahi kuwatimulia vumbi. Wao wanadai kama hanywi angeshuka tu basi anagalau awasalimie na kuwanunulia pombe awaache waendelee kwa furaha zao.
Shango hakuwa mnywaji lakini alikuwa anachukua jagi anazuga kama naye kanywa kwa kuweka mdomoni ilimradi tu achanganyike nao. Sasa Dk. Mwigulu kama yupo hivyo je akija kuwa Rais si ndiyo atakuwa anaishia Singida mjini.