Wanairaimba: Dkt. Mwigulu hatununuliagi hata pombe

No wonder singida bado iko nyuma sana kimaendeleo.
Pombe nayo ni kitu cha kulilia?
 
Wanataka wachapwe bakora walevi hao
 
Kuna hotuba ya kaburu wa Africa kusini, yule rais wa pili kutoka mwisho wa Makaburu, alisema sie watu weusi tunawezaga kucheza ngoma, kua na wanawake wengi, kunywa pombe; akaendelea zaidi kwamba mtu mweusi mwenye akili sana anauwezo wa ku plan jambo kwa miezi 12 tu, hakuna mwenye uwezo wa zaidi ya hapo. Ni matusi kwetu lakini sasa ukisoma ujumbe hu wa wana Iramba, hivi yule Kaburu unamkatalia wapi? Simkubali sana Mwigulu, lakini hoja yao mbona ipo shallow namna hiyo? Yaani mtu awanunulie pombe baasi then? Mi nilidhani kwakua kijana wao kwa sasa ni waziri wa fedha, wangeanza kufanya robbing ili wapate maji, biashara ya vitunguu waanze kuvisafirisha kwenda nje, wawe na maisha mazuri ili iwashawishi hata vijana wao waliopo mjini watamani kurudi nyumbani wakiwa likizo, mabinti zao waache kuchukuliwa kwenda kuuza bar Mwanza, Arusha, Dodoma nk; wao wanataka kununuliwa pombe, wanataka akija wanywe nae pombe? Tumelogwa sisi, sio siri
 
Wanyiramba mtaendelea kuwa masikini sn sababu ya Mwigulu
 
Ndiyo maana Iramba imejaa nyumba za tembe
 
Ndiyo maana Singida huko kumedumaa,kama akili zenywewe ndiyo hizi,bado sana kama kujunuliwa Pombe ni hitaji la msingi,basi kina Mwigulu watatawala milele maana wanaongoza vilaza sana
 
Huu ni ujinga, na hao wapumbavu wanao omba pombe badala ya mambo muhimu kwa maendeleo ya maisha yao.
Ndio Wapiga kura hao, unafikiri wenye uwezo wa kuhoji ya msingi wakiingia site tutakuwa na Wabunge hawa?.

Hapo wamesahau tu kuulizia Tshirt na Kofia...au huenda hizo walizipata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…