MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 350
- 576
Mahakama ya kijeshi, huko DRC, Kivu kusini, leo tarehe 14 Februari 2025, imewahukumu wanajeshi 212 kifo, baada ya kukutwa na hatia ya kukimbia adui,kosa lililotafsiriwa kuwa ni usaliti wa kiapo. Mbali na hukumu hiyo, wote wametakiwa kulipa faini ya dola za kimarekani, laki mbili. Mashitaka yaliyowakabili ni usaliti wa kiapo, wizi wa mali za raia, mauaji ya raia na kubaka wanawake.
Kuna wanajeshi 72 walioachiwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi, huku wengine 90 wakiwa na kesi kama hiyo hiyo huko mjini Uvira.
Hukumu hiyo ilitolewa, M23 ikiwa njiani kuelekea Bukavu mjini, lilipo gereza. Gereza hilo pia mpaka sasa haijafahamika kama wafungwa hawajatoroka.
M23, imekuwa ikisisitiza watu wabaki makazini kwao, wakiwemo askali magereza, kwa sababu inaheshimu katiba ya nchi yao, hivyo wafungwa waliohukumiwa, wanatakiwa kumalizia adhabu zao huko huko gerezani.